Nahodha wa timu ya Liverpool Steven
Gerrard amemshutumu mchezaji mwenzake Mario Balotelli kwa kuonyesha utovu wa
nidhamu pale alipolazimisha apige mkwaju wa penalti badala ya Jordan Henderson
aliyekuwa tayari anakwenda kupiga adhabu hiyo dhidi ya timu ya Besiktas ya
Uturuki.
Balotelli alifunga penalti hiyo na
kuiwezesha Liverpool kuibuka washindi wa bao 1-0 katika mchezo wa ligi ya Uropa
unaozishirikisha timu 32 uliochezwa Alhamisi katika uwanja wa Anfield.
Hali hiyo ilijitokeza baada ya
kushindwa kuelewana na nahodha wa mchezo huo Henderson na Daniel Sturridge juu
ya nani abebe jukumu la kupiga penalti hiyo.
Gerrard amesema: "Henderson ni
nahodha na Balotelli kwa kiasi fulani alionyesha kumkosea adabu katika hali
hiyo."
Gerrard ambaye kwa sasa ni majeruhi,
alikuwa mchambuzi katika matangazo ya mchezo huo kwenye televisheni ya ITV ya
nchini Uingereza.
Steven Gerrard nahodha wa Liverpool
Gerrard amesema kuwa Balotelli alikuwa
"kwa kiasi fulani kakosea" baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa
Italia kumnyang'anya mpira Henderson, ambaye alikuwa amejitayarisha kupiga
penalti hiyo.
Henderson alikuwa nahodha wa
Liverpool dhidi ya Besiktas, na Gerrard anaamini angekuwepo katika mchezo huo
angepiga penalti hiyo.
"Sheria ni sheria,"
amesema. "pongezi kwa Mario, amefunga, lakini si vizuri kuona wachezaji
wakibishana. Nafikiri Jordan alilichukua suala hilo vizuri."
Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers
baada ya mchezo huo hakufafanua nani
RAUNDI YA MTOANO TIMU 32
MATOKEO
Alhamisi Februari 19
Young Boys 1 Everton 4Torino 2 Athletic Bilbao 2
Wolsfburg 2 Sporting Lisbon 0
Aalborg 1 Club Brugge 3
Dnipro 2 Olympiakos 0
Trabzonspor 0 Napoli 4
AS Roma 1 Feyernoord 1
PSV Eindhoven 0 Zenit St Petersburg 1
Guingamp 2 Dynamo Kiev 1
Anderlecht 0 Dynamo Moscow 0
Ajax 1 Legia Warsaw 0
Sevilla 1 Borussia Monchedgladbach 0
Villarreal 2 FC Salzburg 1
Liverpool 1 Besiktas 0
Tottenham 1 Fiorentina 1
Celtic 3 Inter Milan 3
MARUDIANO
Alhamisi Februari 26
20:00 Zenit St. Petersburg v PSV Eindhoven
20:00 Dinamo Moscow v RSC Anderlecht
21:00 ACF Fiorentina v Tottenham Hotspur
21:00 Red Bull Salzburg v Villarreal CF
21:00 Besiktas v Liverpool
21:00 Internazionale v Celtic
21:00 FC Dinamo Kiev v Guingamp
21:00 Legia Warsaw v Ajax Amsterdam
21:00 Borussia Mönchengladbach v Sevilla FC
23:05 Club Brugge KV v Aalborg BK
23:05 Athletic de Bilbao v Torino FC
23:05 SSC Napoli v Trabzonspor
23:05 Olympiacos CFP v FC Dnipro Dnipropetrovsk
23:05 Sporting Lisbon v VfL Wolfsburg
23:05 Feyenoord Rotterdam v AS Roma
23:05 Everton FC v BSC Young Boys
Chapisha Maoni