Na Alex
Mapunda,Iringa
IMEELEZWA
kuwa ili Lipuli iweze kupanda daraja zinaitajika shiringi Milioni 180 au 200 Fedha ambazo zitatumika kwaajili ya maitaji
yote ya timu hiyo.
Akizungumza
na Championi Ijumaa Katibu Msaidizi ya Lipuli Ronjino Malambo alisema bila kuwa
na fedha za kutosha ni ngumu sana kuendesha
timu kwa kuwa toka kipindi cha usajili hadi mwisho wa ligi timu inatumia fedha
muda wote.
“Mara nyingi
tunaendesha timu kwa ahadi hewa bila fedha mfukoni hali ambayo inapelekea
wasamaria wema kuiokoa timu dakika za mwisho kwaajili ya kusafiri au chakula,
kimsingi viongozi tunapata shida jinsi ya kuudumia wachezaji,tunaitaji
kushikamana kwa pamoja”
“Ili kupa
hizo milioni 200 lazima tuungane wote; viongozi,wadau pia ndugu jamaa na
marafiki wa Lipuli na kuhakikisha fedha zinapatikana kwa wakati, watu wanaweza
wakahoji hizo pesa ambazo nimezitaja hapa ni nyingi la hasha! Tunaitaji kuweka
kambi zuri,kusajili wachezaji wazuri na kuwalipa mishahara mizuri” alisema
Malambo.
Pia Malambo
aliongeza kuwa kwa sasa wameanza kukusanya vijana wenye vipaji ambao watakuwa
chini ya mchezaji wa zamani wa timu hiyo Bona Kidava ambao watuungana na wachezaji wengine
watakaosajiliwa toka maeneo tofauti hapa
nchini kwaajili ya msimu mpya.
Timu ya
lipuli imeshindwa kupanda daraja msimu huu baada ya kufanya vibaya katika raundi
ya pili na kuipisha African Sports na Maji Maji
kupanda toka Kundi A ligi daraja
la kwanza ambayo imemalizika hivi karibuni.
Chapisha Maoni