mashabiki wa yanga
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika Yanga kesho wanashuka dimbani kwenye dimba la taifa , Dar es Salaam kupambana na FC Platinum ya Zimbabwe katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya pili ya michuano hiyo .
FC Platinum
Yanga ambayo ndiyo kinara wa ligi ya VodacomTanzania bara ikiwa na pointi 31 imefikia hatua hiyo baada ya kuitoa BDF XI ya Botswana kwa jumla ya mabao 3-2,katika mchezo wa hatua ya awali.
Wapinzani wao FC Platinum ambao wanashiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo baada ya kushika nafasi ya nne kwenye ligi ya Zimbabwe, imefika hatua hiyo baada ya kuitoa Sofa Paka ya Kenya kwa jumla ya mabao 4-2, huku timu hiyo ikishinda mechi zote mbili nyumbani na ugenini.
Changamoto kubwa kwa Yanga itakuwa ni kuwakosa nyota wake watatu akiwepo nahodha wake Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kiungo Mbrazili Andrew Coutinho ambaye anasumbuliwa na matatizo ya enka na Daany Mrwanda ambaye anatumikia adhabu ya kadi nyekundu.
FC Platinum imewasili na kikosi kamili na kocha wake Norman Mapeza, ameahidi kurudi Zimbabwe na ushindi kutokana na namna alivyokiandaa kikosi chake na kuijua vizuri timu ya Yanga kuanzia wakati alipokuwa akicheza hadi sasa amekuwa kocha .
Mapenza aliyewahi kucheza soka la profeshino barani ulaya na ni moja ya kocha mwenye heshima kubwa nchini Zimbabwe baada ya mwaka 2002 kuchukua ubingwa wa ligi ya Zimbabwe akiwa na timu ya taifa ya vijana wenye umri wa miaka 22 na sasa ameichukua timu hiyo ya FC Platnam ikiwa katika hatari ya kushuka daraja kabla ya kuiokoa na kushika nafasi ya nne sasa.
Timu hizo hazijiwai kutana hii itakuwa mechi yao ya kwanza.
Chapisha Maoni