Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars ) Mart Nooj, ametangaza
kikosi cha wachezaji 27 watakaoingia kambini kujiandaa na mchezo wa
kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi utakaofanyika uwanja wa CCM
Kirumba jijin Mwanza Machi 29, 2015.
Taifa
Stars inayotarajia kucheza na The Flames mwishoni mwa mwezi huu,
itaingia kambini machi 22 machi katika hotel ya Tansoma kujiandaa na
mchezo huo kabla ya kuelekea jijini Mwanza machi 24 kwa maandalizi ya
mwisho kabla ya mchezo.
Wachezaji
walioitwa kuingia kambini kujiandaa na mchezo huo ni; Magolikipa,
Deogratius Munish (Yanga), Aishi Manula na Mwadini Ali (Azam FC),
walinzi ni Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris (Azam FC),
Mwinyi Haji (KMKM), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani, Nadir
Haroub, Oscar Joshua (Yanga), Abdi Banda na Hassan Isihaka (Simba SC).
Viungo
ni Frank Domayo, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Mcha Khamis (Azam FC),
Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haroun Chanongo (Stand
United), washambuliaji Mwinyi Kazimoto (Al Markhiry - Qatar),
Saimon
Msuva , Mrisho Ngasa (Yanga), Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta (Tp
Mazembe - Congo DR), John Bocco (Azam FC), na Juma Luizio (Zesco United -
Zambia)
Timu
ya Taifa ya Malawi inatarajiwa kuwasili jijini Mwanza machi 27, 2015
ikiwa na kikosi kamili, wakiwemo wachezaji nane wanaocheza soka la
kulipwa nchini Afrika Kusini, Msumbuji, Congo DR na Zimbambwe.
Malawi
inashika nafasi ya 91 katika viwango vipya vya FIFA Duniani
vilivyotolewa mwezi huu, huku Tanzania ikipanda kwa nafasi saba na
kushika nafasi ya 100.
Chapisha Maoni