Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa siku ya
jumapili kati ya Simba SC na Young African utakaofanyika kwenye dimba la Uwanja
wa Taifa kuanzia majira ya saa 10 kamili za jioni.
Mchezo
huo utachezeshwa na mwamuzi Martin Saanya kutoka Morogoro, akisaidiwa na Soud
Lila (DSM) mshika kibendera wa kwanza, Florentina Zabron (Dodoma) mshika
kibendera wa pili, Mwamuzi wa akiba Israel Mjuni (DSM), na kamisaa wa mchezo ni
Ame Santimeya (DSM).
Viingilio
vya mchezo huo, VIP A sh. 40,000, VIP B sh. 30,000, VIP C sh. 20,000,
Rangi ya Machungwa (Orange) sh. 10,000, huku Rangi ya Bluu na Kijani ikiwa ni
sh. 7,000.
Tiketi
zitaanza kuuzwa keso (jumamosi) saa 2 kamili asubuhi katika vituo vya,
Karume (Ofisi za TFF), Mgahawa wa Steers (Posta Mpya), Oilcom (Buguruni), BigBon
(Kariakoo), Olicom (Ubungo), Dar Live (Mbagala), Uwanja wa Uhuru,
Kivukoni (Ferry) na Makumbusho (kituo cha mabasi).
Magari
yenye vibali maalum ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia ndani ya uwanja siku ya
jumapili kwa kupitia barabara ya Mandela na Uwanja wa Uhuru, barabara ya
Chang'ombe itafungwa kuanzia saa 12 kamili asubuhi.
TFF
inawaomba, wapenzi, washabiki na wadau wa mchezo kununua tiketi katika vituo
vilivyotajwa ili kuepuka kuuziwa tiketi bandia, ili kuimarisha ulinzi na
usalama wa mchezo, mashabiki wenye mabegi, silaha, vilevi na chupa za maji
hawataruhusiwa kuingia navyo uwanjani.
Aidha, katika mchezo huo TFF itatoa ujumbe maalum kupitia kwa wachezaji kuhamasisha juhudi za Taifa za kuzuia mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).
Chapisha Maoni