Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Wachezaji watano wa kilabu ya Kano Pillars nchini Nigeria walipigwa risasi na wapiganaji katika shambulizi lillolenga msafara wa kilabu hiyo wakati wachezaji hao walipokuwa wakielekea Owerri katika mechi ya ufunguzi wa Ligi kuu nchini Nigeria.
''Wachezaji watano walijeruhiwa kutokana na shambulizi la risasi .Wachezaji hao ni Gambo,Ogbonaya,Eneji Otekpa na Murtala Adamu'', ulisema ujumbe wa mtandao wa twitter wa kilabu hiyo.
Wapiganaji hao pia walichukua simu pamoja na vitu vyengine muhimu vya wachezaji hao.
kano Pillar
Mechi iliokuwa ichezwe siku ya jumamosi kati ya timu hiyo na ile ya Heartland imeahirishwa mara moja.
Kilabu hiyo ya Kano Piilars ilikuwa ndani ya basi lililowabeba wachezaji 25,ikiwemo wachezaji 18,wakati wa tukio hilo lililotokea mwendo wa saa saba na robo saa za Nigeria.
kano Pillars
Wachezaji waliojeruhiwa kwa sasa wanaendelea kupokea matibabu katika kituo cha matibabu cha Lokoja.
Siku ya ijumaa beki wa kilabu hiyo Reuben Ogbonnaya aliiambia BBC kwamba anamshukuru Mungu kwa kumuezesha kuishi kwa sababu hajui ni nini kingetokea.


Chapisha Maoni