Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




 
TIMU ya coastal union pamoja na Kagera sugar leo hii zimegawana pointi baada ya kufungana bao 2-2 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa mkwakwani Tanga.

Katika mchezo huo  Coastal union walipata goli la kuongoza katika dakika ya 10 kupitia kwa Selemani Kibuta na kuipeleka mapumziko Coastal union wakiwa mbele kwa goli 1-0.


kipindi cha kwanza Coastal union walicheza kwa kuelewana zaidi kuliko Kagera lakini Kipindi cha pili kilianza tofauti baada ya Salum Mayanja kufanya mabadiliko ambayo yalisabisha goli la kusawazisha kabla ya Coastal union kuandika goli la pili kwa mkwaju wa penati iliyopigwa na Ramadhan Salim katika dakika ya 68.


Alikuwa Rashindi Mandawa aliyeisawazishia Kagera Sugar akitumia juhudi binafsi katika dakika ya 86 na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2.


Chapisha Maoni