UONGOZI wa timu ya soko la Lipuli Fc umewataka wanachama wake na mashabiki kujitokeza kwa wingi leo majira ya saa 4 asubuhi katika mkutano wake utakaofanyika ukumbi wa VETA mjini Iringa.
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa Lipuli Fc Abuu Changawa wakati akizungumza na wanahabari leo kuhusiana na maandalizi ya mkutano huo huku akiwataka wale wote wenye ushauri na maoni mbali mbali kufika ili kueleza ndani ya mkutano huo .
Pia alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kujipanga upya na kuangalia namna gani timu hiyo mwakani anaweza kupanda Ligi kuu baada ya mwaka huu kupoteza nafasi hiyo .
Alisema katika mkutano huo pia wanachama wa kikundi cha Hamsha popo wamealikwa kufika ili kuweza kutoa madai yao mbali mbali dhidi ya uongozi wa Lipuli Fc .
Japo akisisitiza kuwa katika katiba ya Lipuli Fc hakuna kikundi cha Hamsha popo na kuwa kufika kwao katika mkutano huo ni mwanzo wa wao kujipambanua zaidi juu ya namna gani wamekuwa wakiisaidia Lipuli Fc .
Chapisha Maoni