Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Chelsea walitawala kwenye timu bora ya mwaka iliyotangazwa Jumapili na Chama cha Wachezaji Soka Wataalamu, huku wachezaji sita kutoka kwa mabingwa hao watarajiwa wa Ligi ya Premia wakiteuliwa kwenye timu hiyo na wachezaji wenzao Uingereza.
Vijana hao wa Jose Mourinho, waliotoka sare tasa na Arsenal baadaye Jumapili, wamo mbele sana kileleni na wanakaribia kurejesha taji la ligi ya Uingereza Stamford Bridge mara ya kwanza tangu 2010.
Timu hiyo bora ya mwaka ya PFA ilikuwa na wachezaji wanne pekee Waingereza.
Eden Hazard, mmoja wa wanaopigania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa PFA, yumo safu ya kati pamoja na mwenzake Nemanja Matic, huku straika nyota Diego Costa, ambaye amefunga mabao 19 Ligi ya Premia msimu huu kufikia sasa, aliteuliwa safu ya mashambulizi.
Nahodha wa Blues John Terry na mkabaji mwenzake Gary Cahill wamo kwenye safu ya ulinzi ya timu hiyo ya PFA, sawa na mkabaji kabili Branislav Ivanovic .
Ryan Bertrand, mkabaji kamili mwingine aliye kwenye timu hiyo, alikuwa mchezaji wa Chelsea mwanzo wa msimu kabla ya kujiunga na Southampton kikamilifu baada ya kuwa St Mary’s kwa mkopo.
Kipa wa Manchester United David de Gea yuko langoni kwenye timu hiyo. Safu ya kati pia ina nyota chipukizi wa Liverpool Philippe Coutinho na kigogo wa Arsenal Alexis Sanchez.
Nyota wa Tottenham Hotspur anayechezea Uingereza Harry Kane, aliyepigiwa upatu kutawazwa mchezaji bora chipukizi wa PFA kwenye sherehe ya kutoa tuzo jijini London baadaye Jumapili, aliteuliwa kushirikiana na Costa safu ya mashambulizi.
Timu bora ya mwaka ya PFA:
David de Gea (Manchester United); Ryan Bertrand (Southampton), Branislav Ivanovic (Chelsea), John Terry (Chelsea), Gary Cahill (Chelsea); Eden Hazard (Chelsea), Philippe Coutinho (Liverpool), Nemanja Matic (Chelsea), Alexis Sanchez (Arsenal); Harry Kane (Tottenham Hotspur), Diego Costa (Chelsea)


Chapisha Maoni