Kocha anayeondoka wa Borussia Dortmund, Jurgen Klopp ananuia kuharibu ndoto ya watanashari wao Bayern Munich ya kumaliza na mataji matatu musimu huu katika nusu fainali ya kombe la Pokal Jumanne.
Klopp ataongoza timu yake katika uga wa maadui wao Allianz Arena kwa mara ya mwisho baada ya kutangaza atajiuzulu wadhifa wake baada ya miaka saba ya utawala huku akilenga kusema kwaheri na taji Mei 30 katika fainali ya shindano hilo ingawa miamba wa Bayern watakuwa kizingiti kikubwa.
Katika semifainali ya Jumatano, magwiji wa Bundesliga, VfL Wolsburg watamenyana na Arminia Bielefeld wa divisheni ya tatu ambao kufikia sasa, wameangusha majitu kufikia hatua hii.
Bayern wamepanga kumkabidhi Klopp shada la maua kabla ya kipenga cha mwanzo baada ya kuwapokonya taji la Bundesliga 2011 na 12 kabla ya kuongoza Dortmund kumaliza wa pili nyuma yao misumu miwili iliyopita mtawalia.
Lakini Klopp ana haja kubwa ya kuwaharibia azima yao ya kuzoa vikombe vitatu musimu huu katika mechi yao ya kwanza tangu kuhakikishiwa ubingwa wa Bundesliga Jumapili.
“Ni ishara njema sana lakini Jumanne, azima yetu ni kupigana na hatutaki kujizoofisha na maua. Tuko katika kipindi cha lala salama musimu huu na wala si wa kuaga Klopp,” afisa mkuu mtendaji wa Dortmund, Hans-Joachim Watzke alisema.
Kulingana na kiongozi huyo, makubaliano kati yake na mwenyekiti wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge yameafikiana shada hilo litapewa Klopp baada ya mechi.
“Sina shida na hilo na ninaelewa sababu yao ya kupendekeza hivyo,” Rummenigge ambaye alipewa maua katika mechi yake ya mwisho na Dortmund kabla ya kuhamia Munich 1984
Chapisha Maoni