Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


 
Na Alex Mapunda,Iringa
TIMU ya soka ya Maji Maji imefanikiwa kusajili wachezaji wawili toka nje ya Tanzania na wanatarajia kuwasili hapa nchini Aprili 18 kumwaga Wino.
Meneja wa timu hiyo God Mvula amesema wachezaji hao ni Kiungo Kessy Wamwata toka Ghana pamoja na Mshambuliaji Sunday Banda toka Malawi.
Pia Mvula aliongeza kuwa Maji Maji imezamilia kusajili wachezaji wazuri  ili kuleta ushindani mkubwa katika ligi kuu kwa kuwa wamechoka kushiriki katika Madaraja ya chini.
“kila timu inapenda kucheza ligi kuu,na sisi pia tunapenda kucheza ligi kuu tena bila kushuka machungu tuliyopata yanatosha sasa ni mwendo mdundo,Simba,Yanga na Azam watatukoma”alisema Mvula.
Timu ya Maji Maji ni moja ya timu ambazo zilifanya vizuri sana miaka ya 1980 hadi 2000 ambapo ilifanikiwa kuwakirisha nchi katika mashindano ya kimataifa mara tatu mwaka 1985,86 pia 98.


Chapisha Maoni