Kamati ya Mashindano ya TFF ilikutana jana kupitia maandalizi ya
Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) pamoja na taarifa ya Ligi Daraja la Pili (SDL)
iliyomalizika hivi karibuni.
Katika matukio ya SDL, Kamati imeipiga faini ya sh. 300,000 timu
ya JKT Rwamkoma ya Mara kwa kusababisha mechi yake dhidi ya AFC ya Arusha
kuvurugika. Adhabu hiyo kwa mechi hiyo iliyofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 28(4)
ya Ligi Daraja la Pili.
Nao makocha wa JKT Rwamkoma, Hassan Makame na Kamara Kadede
wamepigwa faini ya sh. 200,000 kila mmoja na kufungiwa mechi sita kwa
kumshambulia mwamuzi msaidizi namba moja katika mechi hiyo iliyochezwa Machi 9,
2015.
Wachezaji Shafii Maganga, Saleh Ali, Ismail Salim na Mussa
Senyange wa JKT Rwamkoma ambao wanatuhumiwa kwa kushambulia mwamuzi kwenye
mechi hiyo suala lao linapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa hatua
zaidi.
Chapisha Maoni