Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.





Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine leo amefungua rasmi semina ya waamuzi vijana wenye umri wa miaka 12- 17, inayofanyika katika hostel za TFF zilizopo Karume.


Akizungumza na waandishi wa habari, Mwesigwa amesema semina hiyo ya vijana imejumuisha vijana 27 kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuwaandaa kuwa waamuzi wa kimataifa baadae.

Vijana hawa mnaowaona hapa wanatoka katika viuto vya kufundishia waamuzi vijana nchini, wakikua na kufuata misingi ya kazi baadae watakua waamuzi bor nchini kwa sababu watakua wameanza tangu wadogo na kufuata maelekezo ya wakufunzi wao.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi nchin Bw. Salum Chama akiongea na wandishi wa habari kabla ya kumkaribisha katibu mkuu, amesema malengo yao ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na waamuzi wa kimataifa wengi.

Mwaka huu Tanzania imeshika nafasi ya pili kwa kutoa waamuzi 18 wenye beji za FIFA barani Afrika, nyuma ya Misri yenye waamuzi 22, Lengo ni kuhakikisha tunawaanda vijana wengi waje kuwa waamuzi wa kimataifa.

Semina hiyo ya siku 5 inatarajiwa kufungwa ijumaa tarehe  17 Mei, 2015 inajumuisha vijana kutoka mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Zanzibar, Mwanza, Arusha na Mbeya, kati ya vijana 37 waamuzi wawili ni wanawake.

Wakufunzi wa semina hiyo ni Soud Abdi, Riziki Majala na Joan Minja.


Chapisha Maoni