Aston Villa wamemchukua kiungo wa kati wa Manchester City Scott
Sinclair kwa mkataba wa miaka minne baada yake kufana akiwa huko kwa
mkopo, klabu hiyo ya Ligi ya Premia ilisema Jumanne.
Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea na Swansea City mwenye umri wa miaka 26, ambaye amekuwa Villa Park tangu Januari, amejitolea kukaa katika klabu hiyo iliyofika fainali Kombe la FA, na ambayo sasa haina wasiwasi wa kushushwa daraja na inaweza kuangazia fainali hiyo dhidi ya Arsenal Wembley.
"Nina furaha isiyo na kifani. Tumekuwa na mwisho mwema kwa msimu – sasa naangalia mbele na kusubiri kuanza msimu mpya,” Sinclair, aliyefunga mabao matatu tangu ajiunge na Villa, aliambia tovuti ya klabu hiyo (www.avfc.co.uk):
"Ni vyema pia kwangu na kwa familia kutulia,” akaongeza. “Kwa kila mchezaji soka, ni muhimu kuwa na uthabiti. Ninaamini hili litanisaidia kucheza vyema na kupigania klabu hii kuu miaka ijayo.
"Ni tofauti sana unapokuwa kwa mkopo na unaenda hapa, kulo kila pahali.
"Nimefurahia kila dakika niliyochezea klabu hii. Kuwa mchezaji wa kudumu Villa sasa ni jambo la kunifurahisha sana.”

Chapisha Maoni