Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


 
Arsene Wenger amehimiza vijana wake wa Arsenal waepushe ajali nyingine na kuhakikisha kwamba wanamaliza Ligi ya Premia vyema.
Gunners wamesalia na mechi mbili za nyumbani, dhidi ya Sunderland wanaokabiliwa na hatari ya kushushwa daraja Jumatano na kisha West Bromwich Albion Jumapili, na wanahitaki alama mbili kujihakikishia kumaliza nambari tatu ligini.
Wakishinda mechi hizo mbili wanaweza hata kumaliza nambari mbili ligini baada ya Chelsea, na hiyo itakuwa nambari yao ya juu zaidi katika miaka 10.
Iwapo hawangeshangazwa kwao 1-0 na Swansea City nyumbani wiki iliyopita tayari wangekuwa wamejihakikishia nambari tatu, na Wenger, ambaye bado anapangia fainali ya Kombe la FA, hataki matokeo kama hayo yajirudie dhidi ya Sunderland.
"Tumejitolea sana na itakuwa ujinga sana kutomaliza vyema,” Wenger aliambia kikao cha wanahabari.
“Kwani mechi ya Swansea ilikuwa ajali.
“Sunderland wanahitaji alama moja kuwa salama na hivyo natarajia wajilinde vyema sana, wakae ngumu nyuma, na kujaribu kutumia kaunta, na mipira ya kupangwa, na kufunga mabao.
“Lazima tucheze mechi ya kasi na kucheza kwa nguvu sana kushinda.”
Wenger alisema ni vigumu sana kufikia Manchester City lakini inawezekana.
"Tunaweza tukashinda mechi sita, lakini hazitatosha Man City wakishinda mechi yao ya mwisho dhidi ya Southampton," akasema.
"Kitu kizuri cha kusema ni kwamba inawezekana, kwa hivyo tuna fursa ngapi, sijui, lakini nafasi pekee tuliyo nayo ni kushinda mechi zetu.”
Wenger alikataa kuvutwa kuhusu uvumi unaoendelea kuhusu nyota wa Liverpool Raheem Sterling anayedaiwa kuamua kuhama Anfield.
"Tazama, huwa siwasilishi mambo ya kununua mtu sasa, lakini majira ya joto, tutatafuta kununua wachezaji, ndio. Lakini sasa, akili yangu haiku huko,” akasema.
“Tuna kikosi kikubwa kwa sasa … hatuhitaji wachezaji.
"Ninachotaka ni kumaliza msimu vyema, baadaye nitafanya maamuzi.”


Chapisha Maoni