Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) muda huu inashuka dimbani kucheza mchezo wake wa pili dhidi ya timu ya Taifa kutoka Madagascar, mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Royal Bafokeng majira ya saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Taifa Stars inahitaji kupata ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Madagascar ili kufufua matumaini ya kuweza kusonga mbele katika hatua inayofua ya Robo Fainali.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars akiongelea mchezo wa leo amesema, makosa yaliyojitokeza katika mchezo dhidi ya Swaziland yamefanyiwa kazi na anaamini vijana wake watafanya vizuri.

Aidha Nooij amesema anataarajia mchezo kuwa mgumu kutokana na Madagascar kuhitaji ushindi wa pili mfululizo, baada ya kuifunga Lesotho katika mchezo wa awali, Nooij ameahidi kufanya vizuri katika mchezo huo.


Chapisha Maoni