Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
“Tanzania (Taifa Stars) ilifanya vibaya katika michuano ya Kombe
la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) ilipofungwa kwa aibu katika
hatua ya makundi dhidi ya timu vibonde vya Kundi B; Swaziland (1-0),
Madagascar (2-0) na Lesotho (1-0).”
TANZANIA imeporomoka kwa nafasi 20 katika viwango vya ubora
wa soka vya kila mwezi vilivyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa
(FIFA) leo.
Kwa mujibu wa mtandao rasmi wa FIFA, Tanzania imeporomoka
kutoka nafasi ya 107 iliyokuwa mwezi uliopita hadi nafasi ya 127 ambayo
wamefungana na Vietnam.
Uganda wanaendelea kuongoza Afrika Mashariki wakiwa wameganda
nafasi ya 71 duniani wakifuatwa na Rwanda (94), Kenya (123), Tanzania
na Burundi (134).
10 bora barani Afrika imeendelea kuongozwa na Algeria ambao
wameshuka kwa nafasi moja duniani hadi nafasi ya 21 wakifuatwa na Ivory
Coast (24), Tunisia (29), Ghana (34), Senegal (36), Cape Verde (38),
Nigeria (43), Guinea (45), Congo (47) na Cameroon 49).
Ujerumani imeendelea kuiongoza dunia ikifuatwa na Ubelgiji
waliopanda kwa nafasi moja, Argentina, Colombia, Brazil, Uholanzi,
Ureno, Uruguay, Ufaransa na Hispania wanaokamilisha 10 bora ya dunia.
Nchini hizo vibonde vilivyoing’oa Tanzania COSAFA 2015 zimepanda katika viwango hivyo vya ubora huku moja ikiporomoka.
Swaziland imepanda kwa nafasi 14 hadi nafasi ya 162,
Madagascar imepanda kwa nafasi 37 hadi nafasi ya 113 wakati Lesotho
imeshuka kwa nafasi moja ikiwa nafasi ya 122.
Chapisha Maoni