Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania
(Taifa Stars) Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 23 watakaoondoka leo
jioni kwenda Addis Ababa nchini Ethiopia kuweka kambi ya wiki moja kujiandaa
na mchezo dhidi ya Misri.
Msafara wa Taifa Stars utaongozwa na Wajumbe
wa Kamati ya Utendaji, Vedastus Lufano na Geofrey Irick Nyange “Kaburu” ambaye pia ni Makamu Rais wa klabu ya Simba.
Mchezo kati ya Misri na Tanzania
unatarajiwa kuchezwa Juni 14, katika uwanja wa Borg El Arab jijini Alexandria,
ikiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika (AFCON)
mwaka 2017.
Kikosi cha Stars kinaondoka saa 11 jioni
kwa Shirika la ndege la Ethiopia ambapo inatarajiwa kuwasili jiji la Addis
Ababa majira ya saa 1 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Wachezaji wanaosafiri kuelekea nchini
Ethiopia ni Deogratias Munish, Aishi Manula, Mwadini Ali, walinzi Shomari
Kapombe, Oscar Joshua, Erasto Nyoni, Nadir Haroub, Aggrey Morris, Mwinyi Haji,
Salum Mbonde na Juma Abdul.
Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda,
Salum Telela, Frank Domayo, Jonas Mkude, Said Ndemla, washambuliaji Saimon
Msuva, John Bocco, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta,Mrisho Ngasa na Juma
Liuzio.
Naye mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF Vedastus Lufano amesema timu inakwenda kuweka kambi Ethiopia kwa ajili ya kupambana katika mchezo dhidi ya Misri.
Chapisha Maoni