Sakata la kiungo Ramadhani Singano ‘Messi’ limechukua
sura mpya baada ya Simba kutaka vyombo vya dola kuingilia.
Simba imetaka vyombo vya dola kuingilia na kufanya
uchunguzi ili kuangalia nani aliyefanya fojali kati ya klabu hiyo na kiungo
huyo.
“Sasa tunaomba vyombo vya dola viingilie, wafanye
uchunguzi na mwisho kuwe na ukweli. Sisi tunajiamini na tunataka kusafishwa
katika hili.
“Ndiyo maana tunasisitiza uchunguzi ufanyike kupitia
wataalamu wa vyombo vya dola ili kupata uhakika,” alisema Msemaji wa Simba,
Haji Manara.
Messi amekuwa akilalama kwamba mkataba wake una miaka
miwili na unaisha baada ya kwisha kwa msimu wa 2014-15.
Simba wanapinga na kusema waliingia naye mkata wa miaka mitatu na unamalizika 2015-16. Jambo ambalo limezua malumbano ya kila aina.
Hata hivyo, Simba wamekuwa wakidai wao wana mkataba halisi ambao waliingia na Messi, wakati kiungo huyo amekuwa hana mkataba orijono, anamiliki kopi pekee ambayo inaonyesha ni mkataba wa miaka miwili.
Mkataba wa Singano wasababisha mnyukano mkali Simba, Sputanza wacharuka
‘Kumekuwa na mvutano mkali kati ya Messi na Simba kuhusu madai ya kughushiwa kwa mkataba wa winga huyo.’
CHAMA cha Wachezaji wa Soka Tanzania (Sputanza) kimesema kimewasilisha katika Shiriksho la Soka Tanzania (TFF) nyaraka muhimu kuhusu mkataba wa winga Ramadhani Singano ‘Messi’ na klabu yake ya Simba ili kumaliza mvutano uliojitokeza.
Kumekuwa na mvutano kati ya Messi na uongozi wa Simba baada ya winga huyo kudai kutoutambua mkataba wa miaka mitatu kati yake na klabu hiyo ya Msimbazi uliopo TFF.
Akihojiwa kwenye moja ya vituo vya redio jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Mwenyekiti wa Sputanza, Mussa Kisoky, amesema wamelazimika kuwasilisha TFF nyaraka muhimu za mikataba miwili ya Messi na Simba baada ya kubaini kuna utata katika mkataba wa miaka mitatu ambao mchezaji huyo amedai kutoutambua.
“Messi alifika ofisini kwetu na kutueleza kila kitu kilichotokea kati yake na klabu ya Simba. Kikumbwa ambacho Messi anataka ni ufafanuzi wa mkataba wa miaka mitatu uliopelekwa na Simba TFF ilhali yeye alisaini mkataba wa miaka miwili mbele ya uongozi wa klabu hiyo.
“Baada ya kutupatia nyaraka za mikataba yote miwili, tulibaini kuna utata ndiyo maana tukaamua kuliwasilisha suala hili TFF ili mwanachama wetu (Messi) apate haki yake. Jana nilikaa TFF kwa saa nane tukizungumza nao kuhusu utata wa mkataba wa mchezaji huyu,” amesema Kisoky.
Kiongozi huyo wa Sputanza amefafanua pia mbinu ambazo Messi alizitumia kuingia TFF na kupatiwa nyaraka za mkataba unaodaiwa kughushiwa na Simba.
Amesema kuwa winga huyo alilazimika kumdanganya aliyekuwa Meneja Utawala wa TFF (Wanachama wa Shirikisho), Evodius Mtawala, ili ampatie nakala ya mkataba wake na Simba, jambo ambalo Messi alililifanikisha na kupatiwa nakala inayoonyesha ana mkataba wa miaka mitatu na Simba unaomalizika mwishoni mwa msimu ujao.
Lakini,Messi anadai alisaini mkataba wa miaka miwili na Simba unaomalizika Julai Mosi mwaka huu, jambo ambalo linapihngwa vikali na uongozi wa Simba.
Baada ya maelezo hayo yaliyoonekana kuuumiza uongozi wa Simba, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hanspope, alijiunga moja kwa moja na kipindi hicho cha redio huku akipinga vikali kitengo cha Sputanza kufafanua kuhusu usajili wa Messi redioni kwa madai kuwa mkataba wa mchezaji huyo na Simba ni siri.
“Hayo mambo yote unayoyasema kuhusu kughushiwa kwa mkataba wa Messi bado ni madai. Unayaongea vipi kwenye redio ilhali bado hayajathibitika? Utafanya nini kwa Simba pale itakapothibitika kwamba mkataba wa miaka mitatu uliopo ni halali?” Amehoji Hanspope. Baada ya kuibuka kwa mvutano huyo redioni, Kisoky amesema: “Sijaja hapa kuikandamiza klabu ya Simba, lakini kesi hii itakapoanza TFF, patachimbika mbele ya kamati husika ya TFF.”
Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, baada ya kutafutwa na mtandao huu, alikiri kuzungumza na uongozi wa Sputanza kuhusu sakata hilo, lakini hajapokea rasmi malalamiko yao.
“Ni kweli jana tulikuwa na watu wa Sputanza katika ofisi za TFF na tuliwaambia wawasilishe suala hilo kimaandishi, lakini hadi ninaondoka leo nilikuwa sijaona nyaraka hizo. Huenda wamewasilisha, lakini bado hazijanifikia,” amesema Mwesigwa.
Mvutano wa Messi dhidi ya Simba ni wa kikatiba, hivyo ni wazi utafikishwa mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF.
“SIMBA IMEDANGANYA KUMSOMESHA MESSI
SIKU mbili baada ya Simba kudai
imemsomesha mshambuliaji wake, Ramadhan Singano ‘Messi’, walimu wa shule
aliyosoma ya Al-Farouq Islamic Seminary wameibuka na kukanusha madai
hayo.
Mtandao
huu umefika shuleni hapo na kukutana na mwalimu wa Singano, Abuu Rashid
Laizer anayefundisha masomo ya Historia na Geografia pamoja na mlezi
wake Hashimu Omary Poli.
Shule aliyosoma Singano
Mwalimu
Laizer katika maelezo yake amesema: “Ramadhan Singano amelelewa hapa
kuanzia darasa la pili mpaka anamaliza kidato cha nne mwaka 2010”.
“Hapa
alikuwa analelewa katika idara zote, tukiwa na maana katika malezi yake
kama kijana, kielimu na mambo mengine yanayomuhusu. kwanza ni mtoto
yatima, hana baba wala mama”.
“Shirika
la Africa Muslim Agency lilichukua jukumu kutoka kwa ndugu zake kwa
lengo la kumuwezesha kupata elimu. kama mnavyojua, unapomsaidia yatima
kuna mafanikio ambayo mwenyezi Mungu atakuwezesha mbele ya safari. Moja
ya sera ya shirika ni kusaidia yatima, Ramadhan ni miongoni mwao”
“Kuna vitu vingine watu
wanazungumza labda kutokana na maslahi yao na wanajaribu kupotosha umma,
lakini kiuhalisia huyu bwana (Singano) alikuwa hapa na patroni wake
yupo”.
“Alikuwa
anatokaje hapa mpaka alipoonana na Simba? Wengi wanadhani alitoka Simba
B, lakini Simba walimuona akicheza shuleni kupitia kwa kocha wake
aliyekuwa akiitwa kibonge na aliondoka mwaka 2007 wakati sisi tunaingia.
Licha ya kuondoka, kibonge bado alikuwa na ushirikiano na kijana wetu
pamoja na kaka yake Ramadhan Hamis”.
“Kuna vitu vingine inabidi tuseme
ili tusionekane kumbeba mtu fulani. Mwaka 2007 nikiwa mwalimu wa
michezo nikimsaidia mwalimu anayeitwa Saleh Haruna, nilikuwa nahusika
kutoa vibali kwa Singano kwenda kukutana na wachezaji wenzake wa Simba
B”
“Ni
muda mrefu, lakini imekuja kuonekana hivi juzi kuwa Singano ni moja ya
wachezaji wanaoweza kuisaidia Simba. Kuanzia 2009 mpaka 2011 timu kubwa
iliona anaweza kufaa, lakini yeye ni yatima na wakati anasoma kila kitu
kuanzia kula, kulala mpaka madaftari viligharamiwa na shirika”
“Vitu vyote walikuwa wanapewa na
shirika pindi wakifungua shule. Hakuna mtu aliyekuwa akimlipia ada, mimi
sijaona, labda kama mtu anazo risiti alizokuwa anamlipia alete tuzione
na kuthibitisha”.
“
Utaratibu wetu wa ada ya watoto yatima huwa inakatwa moja kwa moja
Damam, Quwait, ambako ni makao makuu ya Idara ya elimu ya ‘Africa Muslim
Agency’ duniani, lakini kwa Tanzania kuna tawi lake hapa Dar es salaam
na Sheikh Kassim Mzee ndiye aliwatafuta akina Singano na wenzake”.
Baada
ya kuzungumza na mwalimu, tukapata fursa ya kuonana na mlezi wa watoto
yatima shuleni hapo, Hashimu Omary Poli ambaye amefanya kazi toka mwaka
1997 mpaka leo.
Katika malezo yake Poli amefafanuwa kuwa:
“Ramadhan Singano nilimpokea toka
mwaka 2001 akiwa darasa la nne. Amesoma hapa mpaka alipomaliza kidato
cha nne chini ya udhamini wa shirika la Africa Muslim Agency”.
“Kijana
huyu toka alipokuwa mdogo kipaji chake kilidhihirika kwenye suala la
michezo, alionesha uwezo mkubwa na kwa bahati nzuri kulikuwa na mwalimu
Kibonge aliyekuwa karibu nao sana. Mwalimu huyu alipewa fursa kubwa
sana ya kuwa nao na kukuza vipaji vyao”.
“Nashukuru Mwenyezi Mungu mpaka
anafika ‘fomu foo’ alikuwa kijana anayependa sana mpira na akapata
bahati ya kujiunga na Simba. Tukawa tunamsikia Ramadhani Yahya Singano
ni mchezaji na alikuwa anakuja kuwasalimia wenzake na wakati mwingine
anawaletea misaada”.
“Tunashukuru
kwamba anakumbuka fadhila za Maustadh wake, anakumbuka jinsi
alivyolelewa, aliishi na wenzake vizuri, tunamuombea kila la kheri”.
“Ninachokifahamu
mimi kama mlezi nilimpokea akiwa mdogo. Suala zima la kimalezi,
udhamini wa kusomeshwa shule ilikuwa chini ya Shirika la Africa Muslim
Agency. Wao ndio waliomdhamini na walimpokea akiwa mdogo kama wanavyowapokea watoto wengine yatima”. Amesema Poli.
Baadhi ya nyaraka za Singano katika shule aliyosoma
Mwanzoni mwa wiki hii Msemaji wa
Simba, Hajji Sunday Manara alisema klabu hiyo imegharamia masomo ya
Singano na wanashangaa kijana wao kukosa fadhila.
Manara
alisema: “Hivi mnajua Messi tumemtoa wapi Simba? Unajua Ramadhan
Singano amesomeshwa na klabu ya Simba? Mnafahamu hilo? Kasomeshwa IT na
klabu ya Simba, Mnajua fadhila ambayo klabu ya Simba imemfanyia?”
“Hao wanaosema wazazi wake
walikuwa wapi wakati klabu ya Simba inamsomesha? Nauliza, walikuwa wapi?
Klabu ya Simba imegharimia haya. Ninyi waandishi ndio mnaandika vilabu
havithamini wachezaji chipukizi. Sisi ndio klabu pekee yenye wachezaji
zaidi ya asilimia 75 tuliowatoa kwenye mpango wetu wa soka la vijana.
Hawa tunawakuza na bado tunawapa ofa ya usajili”
Singano ameingia kwenye mgogoro na klabu yake akidai imeghushi mkataba wake.
Simba
ina mkataba wa miaka mitatu uliosainiwa mei 1, 2013 na unatakiwa
kumalizika julai 1, 2016, wakati Singano ana nakala ya mkataba wa miaka
miwili aliosaini mei 1, 2013 na unamalizika julai 1, 2015.
Nakala ya mkataba wa miaka mitatu
waliyonayo Simba pia ipo TFF, lakini Singano anadai hakusaini mkataba
huo na anautambua wa miaka miwili.
Licha ya suala hilo la mkataba,
bado Singano hajatimiziwa baadhi ya stahiki zake katika mkataba wake
miaka miwili ikiwemo suala la kodi ya nyumba.
Muonekano wa shule aliyosoma Messi
Chapisha Maoni