Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Barcelona presidential candidate Joan Laporta is keen on bringing Paul Pogba to the Nou Camp if he is elected

Chelsea itamtoa kiungo wake Oscar pamoja na pesa kama sehemu ya dili la kumpata kiungo wa kimataifa wa Ufarasansa na Juventus, Paul Pogba.

Inaeleweka kuwa kocha wa Juventus Massimiliano Allegri ni shabiki mkubwa wa Oscar mwenye umri wa miaka 23 huku Chelsea ikiwa tayari kumwacha aondoke  Stamford Bridge.
Oscar alifunga magoli 6 katika mechi 28 za ligi alizocheza msimu uliopita alishuhudia nafasi yake ya kucheza ikipunguzwa taratibu na sasa huenda akaondoka London.
Chelsea inatarajiwa kupigana vikumbo na  Manchester City, Real Madrid, Barcelona na Paris St-Germain kwa Pobga mwenye thamani ya pauni milioni 70.
Kwa mujibu wa gazeti la Mirror la Uingereza, ni kwamba Mourinho atamtoa Oscar pamoja na pauni milioni 30 ili kunasa saini ya Pobga


Chapisha Maoni