Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu
ya Wanawake wenye umri chini ya miaka 20 (U-20) Tanzanite Stars,
imeingia kambini jana jioni Mbande jijini Dar es salaam na itakua
ikifanya mazoezi katika uwanja wa Azam Complex.
Kikosi cha wacheaji 22 chini ya
Kocha Mkuu Rogasian Kaijage kinafanya mazoezi asubuhi na jioni katika
uwnaja wa Azam uliopo Chamazi kujiandaa na mchezo dhidi ya U-20 ya
Zambia utakaofanyika kati ya tarehe 10, 11 na 12 July jijini Dar es
salaam.
Mchezo huo dhidi ya Zambia ni
wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Wanawake za Dunia wenye umri chini ya
miaka ya 20, zitakazofanyika nchini Papua New Guinea mwaka 2016.
Wachezaji waliopo kambini ni,
Najiati Abbasi, Zuwena Aziz, Shelder Boniface, Stumai Abdallah, Donisia
Daniel, Tatu Iddy (Evergreen Queens), Niwael Khalfani, Maimuna Hamis
(Mburahati Queens), Anastazia Anthony, Amisa Athumani, Amina Ramadhani,
Neem Paulo (JKT Queens).
Wengine ni Asha Shaban, Rebeka
Daniel, Brandina Wincelaus (Tanga), Happines Hezroni, Jane Cloudy (JKT
Queens), Wema Richard, Gerwa Lugomba, Sadda Ramadhani (Uzuri Queens),
Anna Hebron (Evergreen Queens) na Shehati Mohamed (Mburahati Queens)
Aidha wachezaji Monica Henry,
Tumaini Michael (Uzuri Queens), Diana Msewa (Mbeya), na Vailet Nicolaus
(Evergreen) bado hawajaripoti kambini wanaombwa kuripoti na kuungana na
wenzao katika maandalizi ya mchezo huo dhidi ya Zambia.
Chapisha Maoni