Na Alex Mapunda,Iringa
Ramadhani Magoe
"Nilipokuwa nikichezea FC Leopard ya Kenya nilishuudia mchezaji mwenzangu
akichomwa kisu na mashabiki wa Rashavana Fc wakati wakishangiria bao, hali
ambayo ilisababisha kutokea vurugu kubwa na mchezo ukavunjika.
mimi na rafiki yangu tulikimbilia kituo cha polisi ili kuokoa maisha
yetu, baada ya tukio lile wachezaji wenzangu waliniambia yale ni matukio ya
kawaida nchini Kenya kwa vile mfumo wa Kenya ulikuwa ukiruhusu mashabiki
kuingia uwanjani wakati wa kushangilia bao,hata hivyo baada ya kuchomwa kisu Hoteku
alikimbizwa hospitali na kupata matibabu na akapona”.
Hii ni
sehemu ya historia ya maisha ya soka ya Ramadhani Magoe ambaye amevuka milima
na mabonde na kuwa kivutio kikubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki tangu
mwaka 1989 hadi 2012 kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutikisa nyavu na kiburi
uwanjani.
Safari ya
soka ya Magoe ilianza kushika kasi akiwa shule ya msingi Myamatale msoma mjini
toka akiwa mdogo ambapo baada ya kumaliza masomo mwaka 1989 alijiunga na timu
ya tanesco timu ambayo aliichezea kwa misimu miwili na baadae mwka 1992
alinyakuliwa na timu ya Maji Mara klabu ambayo waliipandisha toka ligi daraja
la tatu adi Fainali ya ligi daraja la pili na katika fainali hizo akapata
nafasi ya kusajiliwa na RTC Kagera baada ya wao kuridhika na uwezo wake
wa uwanjani.
Aliitumikia
RTC Kagera hadi mwaka 1996 hapo akatimukia Shinyanga Shooting timu ambayo
aliichezea mechi mbili pekee na akakumbana na kisanga cha kuteguka mguu wakati
wa mechi ya Shinyanga Shoting dhidi ya Milambo ya Tabora tukio ambayo lilimweka
nje ya uwanja kwa kipindi cha mwaka mzima.
Baada ya
mchezaji wa Milambo ya tabora kumtegua mguu alikata tamaa kabisa ya
kuendelea kusakata kabumbu akachukua maamzi magumu ya kurudi kwao msoma na
moyoni alijitangazia kuachana na soka kutokana na mikiki mikiki aliyokutana
nayo baada ya kuteguka mguu.
Lakini mambo
yalikuwa tofauti baada ya kuonana na kocha Silverster Mashiambaye alikuwa
akifundisha timu ya kanisa Viwawa Fc, akanipa moyo na kunishawishi vilivyo na
baadae nikatengua maamuzi yangu na nikaanza kufanya mazoezi katika timu yake ya
Viwawa.
Baadae Mashi
alisajiliwa na timu ya Toto Afrika ya Mwanza na wakati yupo Toto aliwaambia
viongozi wa Toto kuwa Musoma kuna Mashine ya hatari sana tukaichukue ili tuimalishe kikosi chetu,wazo ambalo
Toto waliikubari na waliniitaka kwenda kufanya majaribio,anaeleza Magoe kisha
anaendelea;-
“Nakumbuka
mwaka huo wa 1997 wakati wa majaribio tulikuwa wachezaji 6 wakaongezeka wengine
5,tukapambana na kikosi cha kwanza cha Toto Africa katika mchezo huo tuliibuka
na ushindi mnono wa bao 11-0, mimi peke yangu nilipiga bao 7, wachezaji wa Toto
walikasirika sana kisha wakaomba turudiane ili wapate nafsi ya kusawazisha
hatukufanya ajizi tukawapiga tena bao 8 ambapo mimi nilifunga bao 4 na kupiga
pasi za mwisho.
“Viongozi wa
Toto kulingana na uwezo wetu wakatusajili moja kwa moja na nyota yangu
ilizidi kupeya maeneo yote ya ukanda wa ziwa na viunga vyake ambapo mwaka 1998
alichaguliwa kuchezea timu ya mkoa wa mwanza katika michuano ya Taifa Cup kituo
kilikuwa Kagera nilionyesha kiwango cha hali ya juu sana,na tulitolewa katika
fainali na mzizima United kwa bao 3-2.
“Baada
kumalizika michuano ile nyota yangu iling’aa Zaidi kwa kuwa Nilichaguliwa
kwenye timu ya taifa,piaYanga pamoja na Rtc Kagerawalitanga
kunisajili,kiliochotekea wakati yanga wanataka kunisajili tayari nilikuwa
nimeshamwaga wino RTC Kagera na wakati huo Toto afrika mkataba wangu ulikuwa
umeisha,niliwambia yanga kama wanataka kunichukua wavunje mkataba wangu na
Kagera kitu ambacho walishindwa na nikabakia mikononi mwa RTC Kagera.
“wakati
natumikia timu ya Taifa mechi zangu za mwanzo kuchezea timu ni katika Ufunguza
wa uwanja wa Taifa kwa Sasa unafahamika maarufu kama shamba la Bibi ambapo
Tanzania iliziarika timu kutoka nje ikiwemo Kenya,Uganda,Zambia Pamoja na
Algeria Timu ambazo tulipambana nazo katika sherehe za ufunguzi wa uwanja huo
mimi nikapata nafsi za kucheza mechi za kimataifa kwa mara ya kwanza.
“ndani ya
mwaka huo 1998 nilishuudia mchujo mkali sana ndani ya kikosi cha timu ya Taifa
timu ambayo ilikuwa ikijiandaa na michuano ya awali ya kuuania kufuzu
mashindano ya kumbe la dunia ambayo yalifanyika mwaka 2002 Korea Kusini na
Korea Kaskazini.
“Nakumbuka
tulichukuliwa wachezaji 100 kwenye kikosi cha Taifa baada ya mchujo tulibaki
wachezaji 60,waliongezwa wachezaji wengine 30 toka Zanzibar baada ya mchujo
tulibakia tena wachezaji 60,hiyo haitoshi ulipita mchujo mwingine wa wachezaji
hadi tukabakia wachezaji 30 bora,hata hivyo waliongezwa tena wachezaji 10 toka
mkoani Dar es salam ukafanyika mchujo wa mwisho na tukabakia wachezaji 30
ambapo mimi ingawa nilikuwa mchezaji kijana nilichulikuwa kucheza timu ya
wakubwa na wachezaji wengine ambao walikuwa vijana katika mchujo huo
walipelekwa katika timu ya taifa ya vijana.
“Lakini
licha ya mchujo huu na kuingia kambini huku timu ikiwa na morali ya hali ya juu
tulikung’utwa na Burundi jijini Dar es salam bao 1-0 bao ambalo lilifugwa
dakika ya 80 kwa shuti kali sana toka katikati ya uwanja na Tanzania tukaaga
mashindano,baada ya mchezo ule mashabiki walilizingira basi Letu na wakapasua
vioo kutokana na machungu ambayo waliyapata kwa matokeo mabovu ya mchezo ule na
tuliokolewa na polisi nashukuru mungu hakuna ambaye alipata majeraha makubwa.
“Baada ya
kuitumika RTC kwa Msimu Mmoja mwaka 1999 mwaka ambao baba wa Taifa Rais J
k Nyerere alipoteza maisha nilisajiliwa na FC Leopard ya Kenya wakati huo timu
hiyo ilikuwa chini ya kocha Sundy Kayuni na wakati natua klabuni hapo Timu hiyo
tayari ilikuwa imechukua ubingwa wa Kenya na wachezaji 10 wa timu hiyo walikuwa
wakichezea Timu ya Taifa ya Kenya.
“Basi mvutano
wa kusaka namba katika timu hiyo ulikuwa wa hali ya juu sana ,nakumbuka
nilikuwa nafanya mazoezi mara 4 kwa siku kuanzia saa kumi na moja asubuhi,sasa
mbili,sasa nane pia jioni nilikuwa nikifanya mazoezi ya kukimbia kwaajili
ya Stamina,kutokana na hali hiyo niliimalika Zaidi kimazoezi na nikapata namba
ya kudumu katika kikosi cha kwanza na nilipendwa sana na uongozi wa timu.
“Nilichezea
FC leopard kwa misimu miwili na baadae niliamua kuondoka kwa kuwa viongozi
waLeopard walikuwa wakiitaji mafanikio ya haraka na ndani ya msimu mmoja
walifukuza makocha 7 na yalibuka makundi mawili ndani ya timu hiyo ambayo
yasababisha mvutano mkubwa na ulipelekea viongozi kutwangana makonde kwa hali
hiyo mwaka 2003 nikatimukia Coastal Stars ya Mombasa timu ambayo ilishika
nafasi ya pili na ilipata nafsi ya kucheza michuano ya washindi Afrika.
“Mchuano
ambayo timu yetu ilikumbana na Canon Yaunde Toka comeroon timu ambayo
ilikuwa imetuzidi kwa kila kitu,na hatimaye tulichezea kichapo cha bao 6-0
ambapo mchezo wa kwanza ambao ulipigwa Mombasa tulifungwa bao 2-0 kabla ya
kuchabangwa bao 4-0 nchini comeroon,hali ambayo ilipelekea timu yetu kutolewa
roundi ya kwanza.
“Baaba
mchezo huo viongozi wa timu walianza kusumbua katika maripo ya wachezaji pamoja
na makocha hali iliyosasabisha maisha kwenda kombo,sikuchelewa mwaka 2004
nikarudi Tanzania kukiputa na Toto Africa ya Mwaza timu ambayo nilikaa msimu
Mmoja na baadae mwaka 2005 nilirudi tena Kenya kujiunga na timu ya Sonney
sugar.
“Maisha
ndani ya Sonney Sugar yalikuwa mazuri tulikuwa wanapewa mishahara,posho zuri na
pesa ya kujikimu hasa wakati wa safari na timu yao ilikuwa na uwezo kwa kulaza
wachezaji hadi hoteli ya nyota 5, hivyo wachezaji walikuwa wanajituma sana ili
kupata nafasi ya kusafiri na timu kwa kuwa mpira wa kenya uwezo wako ndio
silaha pekee ya kupata nafasi ya kucheza.
“Niliitumikia
timu hiyo adi mwaka 2009 mwanzoni ambapo kutokana na kusumbuliwa na majeraha
niliamua kurudi Tanzania na nikarudi Msoma kuchezea timu hiyo nikiwa kama
kocha mchezaji na kuipandisha timu hiyo ada ligi daraja la kwanza lakini kuna
mambo yasiyokuwa na kichwa wala miguu yalitokea huku viongozi wa timu hiyo muda
mwingine wakishindwa kusafirisha timu kwa sababu ambazo wanazijua wao
zilinifanya niachane na timu.
“Wakati wa
mashindano ya ligi dala ya kwanza kituo cha Kigoma timu yetu ilikumbwa na
mazingira magumu katika uendeshaji wa mashindano hasa uwajani,kwanza katika
mchezo wa kwanza timu ya polisi ilifanyiwa fitina na waamuzi na ikasababisha
kupoteza mchezo kitu ambacho kilitokea kuna mpira ulipigwa toka winga ya kulia
beki wa timu yetu akapiga mpira kwa goti mwamuzi asema ni penalti,mchezo
mwingine ambao ulikuwa muhimu kwetu ambapo adi dakika ya 80 tulikuwa tukiongoza
bao 2-1 dhidi ya timu toka Kagera mchezaji wetu aliweka mpira kifuani na
mwamuzi akasema amenawa akaamuru ipigwe penalti ikatokea vurugu na mchezo
ukastishwa na wezetu wakachukua pointi tatu.
“Baada ya
matukio yale mimi nikaamua kujiweka pembeni na nikabakia na timu ya Veteran
msoma nikiwa kama mchezaji,lakini baada ya matokeo yale timu ya Polisi Mara
alikabidhiwa Ally Mchumila ambapo aliamua kutumia ushawishi mkubwa ili
kudirudishia katika kikosi hicho nilikataa lakini baadae nilikubali na
niliifungia timu hiyo bao 3 muhimu ambazo ziliipandisha timu hiyo adi ligi daraja
ya kwanza.
“Lakini
baada ya kufanya vizuri uongozi wa timu hiyo ulikosa busara na hekima wakaamua
kumtimua Ally Mchumila kwa kashifa na kibaya zaidi walimleta kocha ambaye uwezo
wake ni mdogo kuliko ule wa Mchumila,na mimi kutokana na kwamba nilikubari
kutumikia timu kwa heshima ya mchumila nikaamua kuachana na timu hiyo na mwaka
2012 nikatangaza kutundika daruga huku bado nikiwa na uwezo mkuwa,aneleza Magoe
huku hakishusha pumzi ndefu kisha anaendelea;-
Woga ulimkimbiza SC Villa ya Uganda Pamoja na Kitwe Wanderers ya Zambia.
“wakati
nilipokuwa RTC Kagera kabla ya kwenda Fc Leopard ya Kenya nilisajiliwa na SC
villa ya Uganda kipindi Villa walikuwa hawakamatiki nilienda hadi uganda baada
ya kukaa pale kwa siku Kadhaa woga ukanijia kutokana na kwamba sikuwa mzoefu wa
kucheza nje ya Tanzania na mazingira ya Uganda yaliniogopesha nikaamua kutoroka
na kurudi RTC Kagera.
“Pia wakati
ligi ikiwa inaendelea timu yetu ilisafiri kucheza mechi za ligi nyanda za
juu kusini katika mikoa ya Iringa,Ruvuma,Iringa,Mbeya na Sumbawanga kumbe
wakati wa ziara hiyo Zambia walituma viongozi wao hapa nchini ili
kunifuatilia,nakumbuka tulipiga kambi Tunduma tukijiandaa na safari ya mkwenda
Sumbawanga.
“Viongozi wa
Kitwe wakanifuata kambini na kunieleza nia yao ya kunisajili niliwakubaria na
baadae nikaondoka nao hadi nchini Zambia nikaenda hadi katika ofsi za timu
hiyo,kwa muda huo tatizo kuwa sikuwa na Vibari vya kuniruhusu kufanya kazi
Zambia baadaye niliwadaganya kuwa wakati utaratibu wa kukamilisha uhamisho
unaendelea waniruhusu nirudi Tanzania na nikawahaidi kurejea Zambia baada
ya siku chache kitu ambacho walilidhia.
“Baada ya
kuondoka nikatokomea mitini kikubwa kilichosababisha ni woga wa kucheza nje ya
Tanzania tatizo likiwa ni kukosa uzoefu katika mechi za kimataifa na
nikarudi RTC Kagera na wazo la Zambia Likapotea moja kwa moja.
Ushirikina michezoni Kenya.
“Kwa kipindi
chote ambacho nimechezea timu za Kenya sijakutana na vitendo vya Imani za
kishirikina wachezaji wa Kenya wanafanya sana mazoezi na uwezo wao uwanjani ni
mkubwa sana kuliko Tanzania timu nyingi za hapa nchini adi zile za vijijini
unakuta adi jenzi za kuvaa siku ya mechi zinalala kwa mgaga wa jadi.
Balaa amecheza ligi Mbili kwa wakati mmoja.
“wakati
nachezea Sonney Sugar ya Kenya mwaka 2005-2009 kuna kipindi nilichezea Timu ya
polisi mara pasipo viongozi wa Sonney Sugara kujua kipindi hicho ligi ya
Tanzania ilichezwa kwa makundi na iliisha kwa muda mfupi.
“kikubwa
kilichonisaidia ni ligi ya Kenya ukishachezea miaka 4 unaruhusikwa kuchaza bila
ITC kwa kuwa tayari unakuwa mchezaji huru na wanakutambua kama mchezaji halali
wanchini hiyo,hivyo unakuwa mchezaji wa kawida na ufuatiliwi,hapo nikapata
mwanya wa kurudi Tanzania na kuchezea timu ya Polisi mara na baadae kurudi tena
Kenya.
Kuchaguliwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya.
“Kocha wa
timu ya Taifa ya Kenya wakati wa michuano mbali mbali ya ligi nchini humo
alitokea kunogewa na kiwango changu na alisahau kuwa mimi ni Mtanzania akaongea
na viongozi wa timu ya FC leopard nia yake ni kuniita katika timu ya Taifa ya
Kenya baada ya kuambiwa mimi ni Mtanzania alisikitika sana.
“Ingawa baada ya kuanza kusakata kandanda nchini Kenya sikupata tena
nafsi ya kutumikia timu ya Taifa ya Tanzania kutokana na ubovu wa techinologia
ya kipindi kile sikufikiria kubadilisha uraia ili kuchezea timu ya Taifa ya
Kenya kutokana na matendo ya kinyama yaliyokuwa yakifanyia uwanjani nchini
Kenya.
“Kuna kipindi nilishuudia watu saba walikufa uwanjani ilikuwa kati ya Gormahia
na FC Leopard hali ambayo ilinisikitisha sana polisi wa Kenya uwanjani walikuwa
wakiweka ulizi kwa wachezaji peke yao mashabiki hata kama wakitwangana
ngumi walikuwa hawaingilii adi yatokee maafa.
“Pia
utamaduni wa wachezaji wa nchini Kenya ni mgumu sana ikilinganishwa na
Tanzania,mnaweza mkalala chumba kimoja kila mtu asubuhi anaamka kivyake hata
salamu hakuna mnakuna mazoezini, kiasi kwamba unaweza ukaumwa usiku na
ukashituka wezako wote wameondoka mara nyingi hata mazoezini tulikuwa
tukiendelea na stori za kawaida bila salama.
“kwa matukio
hayo moyo wangu ulikataa kubadilisha uraia ili kuchezea timu ya taifa ya Kenya
niliogopa wenyeji wangeweza kunifanyia kitu kibaya kulinnga na maisha yao
yalivyo.
Licha ya Masheh kuvukiza ubani Tulilabwa 6-0
“Kiukweli
mpira Burudani kwa kuwa una vimbwanga vingi wakati nasakata kandanda costal
stars ya Mombasa walikuja mashehe wa kiislam siku moja kabla ya kuvaana na
Kanon Yaunde ya comeroon katika kombe la washindi basi usiku kuanzia saa nne
walikuja wazee wa kiislamu na wakapiga dua na kuvukiza ubani hadi usiku wa
manane tukio lile lilituchosha sana wachezaji ukizingati tulilala masaa
machache sana kabla ya mchezo.
“Siku ya mechi kutokana na uchovu tulikimbizwa kama watoto wadogo katika uwanja
wa nyumbani na comeroon wakatukukung’uta bao 2-0 kabla ya kutushushia vua ya
mawe nchini comeroon na kutufungisha vilago pamoja na dua zetu.
Tanzania na ushirikina Damu Damu.
“sisi
Tanzania tunasifika kwa kuwa na matukio ya Imani za kishirikina
michezoni,nakumbuka wakati nachezea timu ya Maji Mara Tulienda katika mashindo
ya kuuania kupanda daraja kwanza katika kituo cha Tabora sisi tulikuwa jukwani
ambapo siku hiyo walicheza kati ya polisi Tabora dhidi ya timu ya
Boma Ulambo ambapo adi kipindi cha kwanza kilipomalizika Polisi walikuwa
mbele kwa bao 2-0.
“kipindi cha
pili yalitokea maajabu ambayo kwangu yalikuwa mageni ambapo upepo ulianza
kuvuma toka kati kati ya uwanja kuelekea golini kwa polisi Tabora na muda wote
wa mchezo walielemewa kiasi kwamba mpira ulikuwa golini kwao,huku boma ya
ulambo wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara na wakafanikiwa kurudisha bao
zote na kuongeza bao la ushindi cha kushangaza mwamzi alipopuliza kipenga
kuashiria mpira umeisha na upepo ukakata huku ulambo wakaibuka na ushindi wa
bao 3-2,hapo ndipo nilipoanza kuamini mambo ya ushirikina uwanjani.
“Tukio
lingine bado tukiwa Tabora timu ya Maji Mara ilichezaja na Shinyanga Shooting
kilichotokea katika mchezo huo waliingia nyuki uwanjani wachazaji wa Maji Mara
peke yake ndio tuliwaona wale nyuki tulijaribu kumweleza mwamuzi alituona kama
watu wa ajabu kwa kuwa yeye hakuwaona wale nyuki wapinzani wetu walitushambulia
sana,kutokana na wale nyuki sisi tulicheza kwa woga na hadi mwisho wa mchezo
Shinyanga shutooting wakaibuka na ushindi wa bao 4-3 na Nyuki wakatoeka
uwanjani.
Soka la kipindi kile na Sasa.
“Soka la
kipindi kile lilitawaliwa na ubabe mwingi pamoja lugha chafu uwanjani beki
alikuwa akikunyajua anakunyanyua kweli muda mwingine ukizubaa mwenzako anaweza
akakuchoma kidole jichoni bila sababu za msingi na sharia zilikuwa ngumu ,beki
amekuchezea faulo mbaya lakini mwamuzi anaendelea na mpira.
“kitu
ambacho kilikuwa kikinisaidia mimi ni kiburi na ngumi kutokana na mazoezi
ambayo nilikuwa nayafanya ilikuwa beki akinizoa mara kadhaa narusha ngumi
muda mwingine mwamuzi alikuwa hatoi kadi hata kama ukirusha ngumi kwa kuangalia
uzito wa faulo uliyokufanyiwa.
“lakini
mpira wa sasa sheria ziko vizuri lakini wachazaji ni wavivu kufanya
mazoezi na kujituma uwanjani ikilinganishwa na sisi kipindi kile.
Jezi yake noma.
“uwezi
kuamini jenzi ambayo ilikuwa ikivaliwa na mimi kipindi kile ilikuwa ngumu
kuvaliwa na mtu mwingine bada ya kuchezea kwa kuwa ilikuwa ikichakaa sana baada
ya kuchezea kutokana kashi kashi za uwanjani.
“mara nyingi
ba
ada ya
dakika 90 nikitoka uwanjani kama sio jenzi basi bukta lazima ichanike,Mabeki
ambao nilikuwa nakutana nao walikuwa wakatili sana ambapo kuchaniwa jezi
ilikuwa ni kitu cha kawaida kwetu sisi washambuliaji.
Adi leo anamwota Ucheche.
Aliyekuwa
beki wa Timu ya Sigara ya Jijini Dar es salam Saidi Ucheche kila nikimkumbuka
alikuwa anatisha muda mwingine adi nacheka peke yangu kwa kuwa Ucheche alikuwa
na mwili kama nyumba,kuna siku tukiwa uwanjani alinipa vitisho akaniambia wewe
dogo unajifanya mjanja leo utaona.
“basi kuna
mpira mmoja ulipigwa juu mimi nikaukimbilia gafla nikasiki kishindo kama cha
gari moshi nikaruka haraka kumkwepa yule bwana kwa jinsi alivyoruka vibaya
endapo ningikutana nae angenitoa meno hata hivyo mwamuzi aliona ikawa faulo.
“zamani mabeki
wazuri walikuwa wengi na walikuwa wakitafuna sana miguu ya washambuliaji na
kikubwa ambacho kilitusaidia ni mazoezi pamoja na ujanja beki mwingine ambaye
nilikuwa namweshimu ni wille Martin.
Wachezaji anaowakubari.
“wachezaji
wa zuri hapa nchini kwa sasa ni wachache sana lakini naheshimu sana uwezo wa
Nurudin Bakari,Athumain Idd [Chuji] Pamoja na Amri Kiemba.
Tukio kali.
“kuna mchezo
ulifanyika mkoani mara kati ya Maji Mara na Duma Fc kuna tukio lilitokea katika
soka hata ulaya halijawai tokea,ilipigwa cross toka winga ya kushoto
kuelekea golini kwa Duma mshambuliaji wa Maji alipiga ule mpira ili
kupasia wavu kitu ambacho kilitokea ule mpira uligonga mwamba kisha mpira
ukapandisha hadi mtambaa wa juu wa goli huku ukiwa unazunguka na kaendelea kuambaa
katika mtambaa wa juu adi mwisho huku wachezaji wa timu zote mbili waliruka
vichwa pale golini baadae mpira ukadondoka upande wa mlingoti wa pili wa goli
na mabeki wakaokoa,tukio hili liliwashitua sana watu.
Makundi 4 ya wachezaji.
“Mpira
haushuki kama roho mtakatifu mpira ni mazoezi na akili ya mchezo,katika mpira
kuna wachazaji wale ambao wanafanya mazoezi ya kocha na mazoezi Binafsi
aina ya wachezaji hao katika mechi mazozini hawachezi vizuri
lakini wanatisha katika mashindano,kundi lingini ni wachezaji wanaotegemea
mazoezi ya mwalimu mechi za mazoezini huwa wanakimbiza sana lakini katika mechi
za mashindano marazote wanachemka.
“kundi la
tatu ni wachezaji wenye uwezo wakunyang’anya mpira uwanjani na kumiliki
mpira wachezaji ambao ni wachache hapa nchini,na kundi la mwisho ni wachzaji
wenye nguvu na uzito wa kutocha ili kujua uzito wa mchezaji uwanjani
unafahamika pindi wachezaji wanapopgongana hapo ndipo mchezaji anaju amegongana
na mtu mwepesi au mzito na ikatokea timu yenu ina wachezaji wachache wenye
uzito mkubwa ushindi kwenu ni maigizo.
“Asilimia
kubwa ya wachezaji tulionao hapa nchini kwa sasa wapokatika kundi la pili ni
wachezaji ambapo wanategeea mazoezi ya mwalimu pekee vile vile hawana uzito wa
kutosha wala uwezo wa kunyang’anya mipira kwa timu pinzani kitu ambacho
kinasababishwa na mazoezi hafifu na wengi wao wamejiingiza katka suala la ulevi
na wanawake.
Makocha.
“TFF
wanadhamana ya kuzalisha makochawa kutosha bila upendeleo na pasipo kujali
maeneo huku mikoani wapo watu wegi ambapo wanaitaji kupata mafunzo na vyeti
bora vya ukocha,bado makocha wengi tuliopo hapa nchini tumepata kozi ya hawali
ambapo tuna vyeti vya kawaida katika mpira.
“Ili kufikia mafanikio katika soka letu lazima tukamilike katika idara zote
hasa idara ya ukocha ambapo mara nyingi tunashuudi wanaletwa walimu toka nje
ambao hawana msaada kwetu,TTF lazima walione hilo.
“ushauri kwa timu ya Taifa & mkoa wa Mara.
“Timu ya
taifa japo kuwa kwa kiasi furani inajitahidi kucheza lakini bado hawafanyi
vinzuri nawashauri TFF warudishe taifa Cup kama ilivyokuwa kipindi kile
ilisaidia sana kupata wachezaji wa timu ya taifa pia wakuze vijana toka chini
ili kuendana na kasi ya soka la kisasa.
“Na ili
kuendeleza soka la mkoani mara viongozi warudishe Imani kwa wananchi kupenda
soka kwa kufanya yale yanayotakiwa katika mpira kwa usahihi,bila hivyo ligi kuu
tutaisikia kwenye Tv,Radio na Magazeti.
Baada ya kustaafu Soka.
“nilizaliwa
mwaka1971 hadi kufikia 2013, nina mke na watoto 6,nafanya biashara ndogo
ndogo pia mimi ni kocha,kikubwa nashukuru mungu maisha yangu ingwa ni ya
kawaida ila ni mazuri yote hayo yametokana na mpira,hivi ndivyo anavyoitimisha
Magoe katika simulizi ya maisha yake ya soka baada ya maojiano maalum na
gazeti namba moja la michezo na burudani hapa nchini nazungumzia Championi.
Chapisha Maoni