Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Kazi ipo! Kikosi cha timu ya taifa ya wanawake cha Twiga Stars kitacheza michuano ya All African Games kikiwa kundi A.
Kundi hilo lina timu za Nigeria, Ivory Coast na Congo Brazaville ambao ndiyo wenyeji.
Michuano hiyo itaanza Septemba 4 hadi Septemba 15, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kintele jijini Brazaville.
Nchi 52 za Bara la Afrika zitashiriki katika michuano hiyo inayoshirikisha zaidi ya michezo 10.
Timu zote zina uzoefu mkubwa wa michauno ya kimataifa, hivyo Twiga italazimika kupambana vilivyo.

Toka TFF


Chapisha Maoni