Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface
Mkwasa leo ametangaza kikosi cha wachezaji 29 watakaongia kambini siku
ya Jumapili tarehe 9, Agosti katika hoteli ya Tansoma iliyopoe eneo la
Gerezani kwa ajili ya kambi ya wiki moja ya mazoezi.
Katika
kikosi hicho alichokitangaza cha wachezaji 29, Mkwasa amewajumuisha
wachezaji watano wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi (Proffesional),
ambao baadae watajumuika kwa kambi ya kujiandaa kucheza na Nigeria mwezi
Septemba 2015 nchini Uturuki.
Taifa
Stars inatarajiwa kuweka kambi ya siku kumi jijini Istambul - Uturuki,
ambapo itacheza michezo miwili ya kirafiki na timu za Taifa za Libya na
Kuwait kabla ya kurejea nchini kuwavaa Nigeria.
Wachezaji
watakaongia kambini jumapili ni magolikipa, Ally Mustafa (Yanga SC) na
Aishi Manula (Azam FC), walinzi wa pembeni: Shomari Kapombe (Azam FC),
Michael Aidan (Ruvu Shooting), Juma Abdul, Mwinyi Haji (Yanga SC) na
Abdi Banda (Simba SC).
Walinzi
wa kati; Hassan Isihaka (Simba SC), Nadir Haroub, Kelvin Yondani (Yanga
SC), Viungo wakabaji: Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya (Azam
FC), Viungo washambuliaji ni Salum Telela (Yanga SC) na Said Ndemla
(Simba SC).
Washambuliaji
wa pembeni; Orgenes Mollel (Aspire – Senegal), Abdrahman Mbambi
(Mafunzo), Deus Kaseke, Saimon Msuva (Yanga SC), Ramdhani Singano, Farid
Musa (Azam FC), huku washambuliaji wa kati wakiwa ni John Bocco, Ame
Ally (Azam FC) na Rashid Mandawa (Mwadui FC).
Chapisha Maoni