MCHEZO wa ufunguzi wa ligi kuu ya vodacom ambayo itaanza kutimua vumbi Septemba 12 INAFUNGULIWA LEO KWA mechi kali kati ya yanga na Azam Fc.
Msimu uliopita, kwenye Mechi kama hii, Yanga iliichapa Azam FC mabao 3-0 kwa Bao za Mbrazil Geilson Santos 'Jaja', Dakika ya 56 na 66, na Simon Msuva, Dakika ya 87.
Azam FC wanatinga Mechi hii wakiwania kutopoteza Mechi ya Ngao ya Jamii kwa mara ya 3 mfululizo baada ya kufungwa na Simba na kisha Yanga mara mbili mfululizo.
Baada ya Mwezi uliopita kutwaa Kagame Cup, wakisimikwa kama ndio Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na ya Kati, Azam FC ya safari hii chini ya Kocha Mwingereza Stewart Hall imeimarika zaidi huku wakitumia Mfumo mpya wa 3-5-2 badala ya ule wa 4-3-3.
Mara ya mwisho kwa Timu hizi kukutana ni hapo Julai 29 kwenye Robo Fainali ya Kagame Cup na Azam FC kufanikiwa kuingia Nusu Fainali walipoitoa Yanga kwa Penati 5-3 kufuatia Sare ya Dakika 90 ya 0-0.
Kwenye Mechi hiyo, katika Mikwaju ya Penati Tano Tano, Kipa wa Azam FC Aishi Manula aliokoa Penati iliyopigwa na Mwinyi Mngwali na Aggrey Morris kuifungia Azam FC Penati ya mwisho na kuipa ushindi.
Penati nyingine zilipigwa na kufungwa na Kipre Tchetche, Wawa, John Bocco na Himid Mao kwa Azam FC wakati za Yanga zilifungwa na Nadi Haroub 'Cannavaro', Salum Telela na Godfrey Mwashiuya.
NGAO YA HISANI-Agosti 22, Saa 10 Jioni, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
VIINGILIO:
-MAJUKWAA KIJANI, BLUU & RANGI YA CHUNGWA: Sh 7,000/=
-VIP B & C: Sh 20,000/=
-VIP A: Sh 30,000/=
Kila Timu ilikuwa kwenye Mazoezi makali ambapo Yanga, chini ya Kocha Mholanzi Hans van Pluijm, ilikuwa huko Tukuyu, Mkoani Mbeya ambako pia ilicheza Mechi za Kirafiki na Juzi kuifunga Mbeya City Bao 3-2 huko Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya kwa Bao za Andrey Coutinho, Amisi Tambwe na Donald Dombo Ngoma.
Nao Azam FC walikuwa huko Visiwani Zanzibar na Juzi waliichapa JKU 2-0 kwa Bao za John Bocco na Salum Abubakar.
Awali Mechi hii ilikuwa ichezeshwe na Refa Israel Nkongo lakini, baada ya kupata maumivu ya Musuli za Pajani, TFF ikambadili na kumtaja Martin Saanya kuwa ndio Mwamuzi wa Mechi hii.
Falsafa za makocha:
Kocha wa Azam, Stewart Hall:
Tangu kurejea kwake Azam kumekuwa na utofauti mkubwa kwenye kikosi cha
hicho ambapo kwa sasa wanacheza mpira wa kasi na kushambulia sana hasa
kupitia pembeni kwa kuwatumia Shomari Kapombe na Michael Gadiel. Lakini
eneo la ulinzi limeonekana kuimarika zaidi na hiyo ilidhihirika kwenye
michuano ya Kagame ambapo Azam haikuruhusu goli hata moja tangu kuanza
hadi kumalizika kwa michuano hiyo.
Ukuta wa Azam unatengenezwa na
Wawa akishirikiana na Agrey Morris, wakati Mugiraneza, Domayo, Himid Mao
wakitarajiwa kuongoza safu ya kiungo na John Bocco pamoja na Kipre
Tchetche wao watakuwa wakicheza kama washambuliaji.
Mfumo wa Azam FC: 3-5-2
Kocha wa Yanga, Van Pluijm:
Anapenda soka la pasi nyingi fupifupi na kushambulia muda wote,
mashambulizi ya timu yanatengenezwa na viungo wa katikati na mara kadhaa
viungo wa pembeni ambao kwa sasa wanaopewa nafasi kucheza nafasi ya
viungo wa pembeni ni wachezaji wapya Godfrey Mwashiuya na Deus Kaseke.
Amis Tambwe na Dolnald Ngoma ni
washambuliaji ambao maranyingi wanapewa nafasi ya kucheza pamoja wakati
safu ya ulinzi ya Yanga ikiongozwa na mabeki wawili wakongwe, Kelvin
Yondani na Nadir Horoub ‘Cannavaro’ wakati Niyonzima akipewa majukumu ya
kuongoza safu ya viungo wa kati.
Mfumo wa Yanga SC: 4-4-2
Wachezaji wakuchungwa kwenye mchezo wa leo:
Yanga: Wachezaji wakuchungwa kwa
upande wa Yanga ni Donald Ngoma, Amis Tambwe, Deus Kaseke, Mwashiuya na
Busungu. Wachezaji hao wote walionesha kiwango kizuri kwenye michuano ya
Kagame japo walitolewa na Azam kwenye hatua ya robo fainali.
Azam: John Bocco amekuwa akifunga
sana kwenye mechi za Simba na Yanga, hivyo Yanga wanapaswa
kuwanayemakini muda wate. Kipre Tchetche, Gadiel Michael ni wachezaji
wengine wanaohitaji uangalizi wa hali ya juu.
Wachezaji wapya ambao wanaweza kupewa nafasi kwenye mechi ya leo.
Yanga: Kuna wachezaji wapya
wawili wa Yanga ambao wamecheza mechi za kirafiki lakini mashabiki
wanahamu kubwa kuwaona leo kwenye mechi ya Ngao ya Jamii, kiungo
aliyenunuliwa kutoka FC Platinum ya Zimbabwe Thaban Kamusoko na mlinzi
wa Togo Vincent Bossou ambao leo wanaweza kupewa nafasi kwenye kikosi
cha Van Pluijm.
Azam: Ramadhani Singano ‘Messi’
ni mchezaji wa zamani wa Simba kila mtu anajua uwezo wake awapo
uwanjani, mchezo wa leo Messi anaweza akapewa nafasi ya kuonesha uwezo
wake akicheza kwa mara ya kwanza mechi ya mashindano akiwa na klabu ya
Azam. Wachezaji wengine wapya waliosajiliwa na Azam wameshapata nafasi
ya kucheza isipokuwa kwa mshamuliaji Alan Wanga ambaye yupo nyumbani
kwao kwenye msiba wa mama yake.
Historia ya Azam na Yanga kwenye kombe la Ngao ya Jamii:
Azam haijawahi kutwaa Ngao ya
Jamii, mara zote ilizopata nafasi ya kucheza kuwania taji hilo imepoteza
mechi zote na kutoka mikono miupu. Mara ya mwisho timu hizo kukutana
kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ilikuwa ni msimu wa 2014-2015, Yanga
ilishinda kwa goli 3-0 na kutwaa taji hilo.
Matokeo ya mechi tano zilizopita kati ya Yanga SC dhidi ya Azam FC
Julai 29,2015: Azam 0-0 Yanga ( penati: Azam 5-3 Yanga)
Mei 6, 2015: Yanga 1-2 Azam
Desemba 28, 2014: Azam 2-2 Yanga
Machi 19, 2014: Yanga 1-1 Azam
Septemba 22, 2013: Azam 3-2 Yanga
YANGA: Ali Mustafa Mtinge "Barthez", Juma Abdul Japhary, Mwinyi Haji Ngwali, Kevin Patrick Yondani "Cotton", Vicent Bossou, Thabani Kamusoko "Rasta", Simon Happygod Msuva, Haruna Niyonzima "Fabregas", Amissi Jocelyn Tambwe, Donald Dombo Ngoma, Andrey Coutinho
AZAM FC: Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Shah Farid Musa, Agrey Morris, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Jean Mugiraneza, Himid Mao, Franky Domayo, John Bocco, Kipre Tchetche
REFA: Martin Saanya
LIGI KUU VODACOM
RATIBA-Mechi za ufunguzi
Jumamosi Septemba 12
Ndanda v Mgambo Shooting (Nang’wanda - Mtwara)
African Sports v Simba SC (Mkwakwani - Tanga)
Majimaji v JKT Ruvu (Majimaji - Songea)
Azam FC v Tanzania (Azam Complex – Dar es Salaam)
Stand United v Mtibwa Sugar (Kambarage - Shinyanga)
Toto Africans v Mwadui (CCM Kirumba - Mwanza)
Jumamosi Septemba 12
Yanga v Coastal Union (Taifa – Dar es Salaam).
Chapisha Maoni