Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetuma
salam za rambi rambi kwa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Pwani (COREFA)
kufuatia kifo cha mwamuzi mstaafu wa mpira miguu Rajabu Zarara kilichotokea
juzi usiku jijini Dar es Salaam.
TFF pia imetuma salam za rambi rambi kwa Mwenyekiti wa
klabu ya Yanga, kufuatia kifo cha mwanachama wake Athuman Makaranga
kilichotokea leo asubuhi jijni Dar es salaam.
Makaranga alikuwa ni mwanachama wa klabu hiyo miongoni
wa wadau wa mpira wa miguu, ambapo alishiriki vyema kwenye michuano ya Kagame
iliyomalizika hivi karibuni.
TFF kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini inawapa pole wafiwa, ndugu, jamaa na marafiki wote kufuatia misiba hiyo na kusema iko pamoja nao katika kipindi hiki cha maombolezo.
Chapisha Maoni