Neymar anavaa jezi namba 10.
Wayne Rooney anavaa jezi namba 10
Washindi wa hivi karibuni wa Ballon d’Or wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia Michael Owen, Ronaldinho Gaucho na Ricaldo Kaka wote walikua wakivaa jezi namba 10.
Moja ya kukua kwa umaarufu wa jezi no. 10 ni kuwahi kuvaliwa na wachezaji bora wa muda wote Ulimwenguni, Pele pamoja na Diego Armando Maradona.
Hilo limechangia kwa kiasi kikubwa jezi hii kuwa na mvuto wa aina yake na kupendwa na mastaa wengi wa soka.
Lakini sababu nyingine ambayo ndiyo ilikua chanzo cha Pele na Maradona kuvaa jezi hiyo kubwa kabisa katika soka ilikuwa ni utamaduni wa kawaida wa kupanga first eleven.
Katika kikosi cha wachezaji 11 wa kwanza, jezi ziligawiwa kuanzia yenye namba ndogo kutoka kwa golikipa hadi kwa mchezaji wa misho namba 11 kulingana na nafasi uwanjani.
Hivyo automatic kutokana na position zao, Pele na Maradona wakajikuta wakigawiwa jezi namba 10 kama washambuliaji wa timu zao.
Mfumo wa mpira ulipobadilika na kuwa 4 4 2 uliwafanya washambuliaji wa mbele wawili mmoja kuvaa jezi namba 10 na mwingine namba 9. Hali hii ikasababisha pia jezi namba 9 kuwa pia na umaarufu wa aina yake. Inavaliwa na Luis Suarez, Samuel Eto’o akiwa Barcelona pamoja na Ronaldo De Lima.
Lakini mabadiliko hayo ya jezi yamepelekea wachezaji wengine kuchagua jezi zenye namba kubwa zaidi ya zilizopo ndani ya 11. David Beckham alichagua jezi no.23 alipotua Madrid na amestaafu akivaa hiyo.
Picha: Magwiji wa soka wenye jezi nambari 10 mgongoni
Chapisha Maoni