Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Amani ukiwa maalum kwa maandalizi ya Twiga Stars kushiriki Michezo ya Afrika (All African Games) hapo baadae, wageni Kenya walikuwa wa mwanzo kupata goli katika dakika ya 42 kupitia kwa Tabatha Chacha.
Twiga stars walisawazisha goli hilo katika dakika ya 62 na kupelkea mchezo kumalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1.
Twiga stars imeweka kambi visiwani Zanzibar ikiwa sehemu ya maandalizi ya kushiriki michezo ya Afrika hapo baadae mwaka huu.
CHANZO SOKA IN BONGO.
Chapisha Maoni