Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




MSHAMBULIAJI Msenegali, Pape Aboulaye N’daw amekamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni Simba SC baada ya kusaini Mkataba  kufuatia kufuzu majaribio.


N’daw aliyejaribiwa katika michezo miwili ya kirafiki dhidi ya JKU Simba ikilala 2-0 Jumamosi na Mafunzo, Wekundu wa Msimbazi wakishinda 3-1 jana, amempiku Makan Dembele kutoka Mali ambaye alitaka kusajiliwa bila majaribio.
 
Na sasa mchezaji huyo wa zamani wa Dinamo Bucuresti ya Romania anaungana na kipa Vincent Angban kutoka Ivory Coast, mabeki Emery Nimubona wa Burundi, Juuko Murushid, washambuliaji Simon Sserunkuma, Hamisi Kiiza wote wa Uganda na kiungo Justuce Majabvi wa Zimbabwe.


Chapisha Maoni