Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Klabu ya Azam FC, imeeleza
masikitiko yake kutokana na
beki Juma Nyosso kumshika
makalio nahodha wake, John
Bocco kwa lengo la
kumdhalilisha.

Jaffar Iddi amesema
wamesikitishwa kwa kiasi
kikubwa na kitendo hicho
cha Nyosso ambacho
kilinaswa na vyombo
mbalimbali.

Nyosso alifanya makusudi
kumdhalilisha Bocco hii
ikiwa ni mara ya pili
kunaswa na vyombo vya
habari akifanya hivyo.
Msimu uliopita alimfanyia
hivyo, Elius Maguri wakati
akiitumikia Simba.
“Vitendo kama hivyo kama
alivyofanya Nyosso
havikubaliki hata kidogo,
tunaalani kwa nguvu zote
kabisa.
“Lakini tunavishukuru
vyombo vya habari kuhusiana
na hilo, vimekuwa shahidi
wa kila kitu. Lakini pia
tunaiachia TFF, tunajua
hadi Rais wa TFF, Jamal
Malinzi hilo limemfikia.
“Tunaamini hatua kali
zitachukulia kukomesha
vitendo kama hivyo visivyo
vya kiungwana,” alisema.
Baada ya kubainika
alimfanyia hivyo Maguri,
Nyosso ambaye ni beki wa
zamani wa Simba, alifungiwa
mechi nane.

Saleh ally



Chapisha Maoni