Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Ushindi wa mabao 2-0 wa
Yanga dhidi ya Simba juzi
kwenye mechi ya Ligi Kuu
Bara, umewafanya wakombe
mamilioni.
Yanga ilionja uhondo wa
kuifunga Simba kwa mara ya
kwanza tangu Mei 18, 2013.
Kwa mujibu wa chanzo cha
habari kutoka ndani ya
uongozi wa timu hiyo,
wachezaji na benchi la
ufundi la timu hiyo
wamepewa kiasi cha shilingi
milioni 40 kama posho baada
ya ushindi huo.
Chanzo hicho kilisema,
wachezaji hao wamepewa
kiasi hicho cha fedha
kutoka kwa mwenyekiti wa
timu hiyo, Yusuf Manji.
Kiliongeza kuwa, mgawo huo
wa fedha hizo utawahusisha
wachezaji wote na viongozi
wa benchi la ufundi la timu
hiyo.
“Kufuatia ushindi
walioupata wachezaji wetu
kwa kushirikiana na benchi
la ufundi, tumepanga kuwapa
kiasi cha shilingi milioni
40 kama zawadi.
“Hiyo ni kama morali na
pongezi kwa wachezaji wetu.
Tuna kazi kubwa katika
kuhakikisha tunatetea
ubingwa wa ligi kuu,
ninaamini hilo linawezekana
kutokana na uwezo mkubwa wa
wachezaji wetu,” 


Na saleh jembe



Chapisha Maoni