Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


KOMBE LA DUNIA 2018
Marekani ya Kusini-Mechi za Mchujo
Saa za Bongo (Mechi hizi kuchezwa Usiku wa
Leo Jumanne kuamkia Jumatano)
Jumatano Oktoba 14
0001 Ecuador v Bolivia
0200 Uruguay v Colombia
0400 Brazil v Venezuela
0400 Paraguay v Argentina
0515 Peru v Chile

Vigogo wa Marekani ya Kusini, Brazil na
Argentina, Leo Usiku wana kazi kubwa ya kufuta
vipigo toka Mechi zao za kwanza za Kanda ya
Marekani ya Kusini kuwania kucheza Fainali za
Kombe la Dunia huko Russia Mwaka 2018.
Ijumaa iliyopita, Brazil ikicheza Ugenini huko
Santiago ilipigwa 2-0 na Chile wakati Argentina,
wakiwa kwao Buenos Aires, walichapwa 2-0 na
Ecuador.
Katika Mechi hizo Brazil ilimkosa Kepteni wao
Neymar ambae yuko Kifungoni na Argentina
ilimkosa Kepteni wao Lionel Messi ambae ni
Majeruhi.
Wachezaji wote hao watazikosa Mechi za Leo
lakini kwa Neymar hii itakuwa Mechi yake ya
mwisho ya Kifungo chake cha Mechi 4.
Leo Brazil wako kwao kuivaa Venezuela ambayo
Wiki iliyopita ilichapwa 1-0 na Paraguay.
Argentina wao Leo watakuwa Wageni wa
Paraguay ambao huwa na kawaida wa kuivimbia
Argentina ambayo Leo itaongozwa na Carlos
Tevez.
KOMBE LA DUNIA 2018
Marekani ya Kusini-Mechi za Mchujo
MATOKEO
Alhamisi Oktoba 8
Bolivia 0 Uruguay 2
Colombia 2 Peru 0
Venezuela 0 Paraguay 1
Chile 2 Brazil 0
Argentina 0 Ecuador 2



Chapisha Maoni