Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
(VPL) inatarajiwa kuendelea
wikiendi hii kwa michezo sita
kuchezwa katika viwanja
mbalimbali nchini, ikiwa katika
mzunguko wa saba timu 14
zitapambana kusaka pointi 3
muhimu.
Young Africans watawakaribisha
Azam FC katika uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam siku ya
Jumamosi, huku timu zote zikiwa
na pointi 15 kileleni
zikitofautiana kwa magoli ya
kufunga na kufungwa.
Kabla ya mchezo wa Yanga dhidi
ya Azam, kutakua na mchezo wa
utangulizi wa kuombea amani
kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa
Rais, Wabunge na Madiwani
utakaofanyika Oktoba 25, 2015.
Mchezo huo utawakutanisha
viongozi wa dini watakocheza
dhidi ya mabalozi wanaofanya
kazi nchini, mechi hiyo itaanza
saa 8:25 mchana na kumalizika
saa 9:15 alasiri.
Majimaji FC ya mkoani Ruvuma
watakua wenyeji wa African
Sports kwenye uwanja wa Majimaji
mjini Songea, huku Ndanda FC
wakiwakaribisha Toto African
kutoka jijini Mwanza katika
uwanja wa Nangwanda Sijaona
mjini Mtwara.
Jijini Mbeya, watoza ushuru wa
jijini hilo Mbeya City FC
watawakaribisha Simba SC katika
uwanja wa Sokoine, Chama la wana
Stand United watakuwa wenyeji wa
Tanzania Prisons uwanja wa
Kambarage mjini Shinyanga, huku
Coastal Union wagosi wa kaya
wakiwakaribisha wakata miwa wa
Mtibwa Sugar katika uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga.
Ligi hiyo itaendelea Jumapili
kwa michezo miwili kuchezwa,
Mgambo Shooting watakua wenyeji
wa Kagera Sugar katika uwanja wa
Mkwakwani, huku Mwadui FC
wakicheza na maafande wa JKT
Ruvu katika uwanja wa Mwadui
Complex.
Asante kwa kutembelea Hope FM Iringa, Asante kwaku-share habari hii, Kama una Maoni, Ushauri, Story ya ku-share na sisi na au Unahitaji msaada...!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni