KOMBE LA DUNIA 2018
Saa za Bongo [Mechi kuchezwa Usiku wa Leo
Jumanne kuamkia Jumatano]
Jumatano Oktoba 14
Ecuador 2 Bolivia 0
Uruguay 3 Colombia 0
Brazil 3 Venezuela 1
Paraguay 0 Argentina 0
Peru 3 Chile 4
Baada ya kupigwa katika Mechi za kwanza
Ijumaa iliyopita, Vigogo wa Marekani ya Kusini,
Argentina na Brazil, Jana waliingia tena dimbani
kucheza Mechi zao za pili za Kanda ya Nchi za
Marekani ya Kusini za kusaka nafasi za
kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka
2018 huko Russia na Brazil kuibuka kidedea
wakati Argentina wakiambua Sare.
Brazil, wakicheza kwao huko Estádio Plácido
Aderaldo Castelo, Mjini Castelo, waliichapa
Venezuela 3-1 huku Bao zao zikifungwa na
Willian Borges Da Siva, Dakika ya 1 na 42 na
Ricardo Oliveira Dakika ya 74 wakati Bao la
Venezuela likifungwa na Christian Santos katika
Dakika ya 64.
Brazil walicheza bila ya Kepteni wao Neymar
ambae ndio alikuwa akimaliza Kifungo chake
cha Mechi 4.
Nao Argentina, wakicheza Ugenini bila ya
Kepteni wao Lionel Messi, waliambua Sare ya
0-0 walipocheza na Paraguay.
Nazo Uruguay na Ecuador zimeendeleza ushindi
baada y azote kushinda Mechi zao za pili hapo
Jana.
Ecuador iliichapa Bolivia 2-0 kwa Bao za Miler
Bolanos, Dakika ya 81, na Penati ya Dakika ya
90 ya Felipe Caicedo.
Uruguay waliichara Colombia 3-0 kwa Bao za
Diego Godin, Diego Rolan na Abel Hernandez
katika Mechi ambayo Colombia walimaliza Mtu
KOMBE LA DUNIA 2018
Marekani ya Kusini-Mechi za Mchujo
MATOKEO
Alhamisi Oktoba 8
Bolivia 0 Uruguay 2
Colombia 2 Peru 0
Venezuela 0 Paraguay 1
Chile 2 Brazil 0
Argentina 0 Ecuador 2
Chapisha Maoni