Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
amesema timu ya soka ya taifa, Taifa
Stars ina mtihani mgumu mbele ya
Algeria.
Taifa Stars inamenyana na Algeria,
mwezi ujao katika hatua ya mwisho
ya mchujo ya kuwania kupangwa
kwenye makundi ya kuwania tiketi ya
Fainali za Kombe la Dunia mwaka
2016 Urusi.
Na akizungumza katika hafla ya
kupongezwa kwake na Wanamicheo
juzi ukumbi wa Mlimani City, Dar es
Salaam iliyoandaliwa na Chama cha
Waandishi wa Habari za Michezo
Tanzania (TASWA), Rais Kikwete
alisema kwamba Algeria ni timu nzuri.
Alisema Algeria ndiyo timu ya Afrika
iliyofanya vizuri zaidi ya zote kati ya
zilizoshiriki Fainali za Kombe la Dunia
mwaka jana Brazil, nyingine zikiwa ni
Ivory Coast, Ghana, Nigeria na
Cameroon.
Kwa sababu hiyo, Rais Kikwete
amesema huo ni mtihani mgumu kwa
Taifa Stars, ingawa ameitakia kila la
heri timu hiyo kuelekea mchezo huo.
Tanzania imeitoa Malawi katika hatua
ya kwanza ya mchujo kuwania
kupangwa kwenye makundi ya
kuwania tiketi ya kucheza Fainali za
Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi
kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda
2-0 nyumbani na Jumapili kufungwa
1-0 Blantyre.
Na baada ya matokeo hayo, Taifa
Stars itamenyana na Algeria katika
hatua ya mwisho ya mchujo, mechi ya
kwanza ikichezwa Dar es Salaam
Novemba 14 na marudiano Novemba
17 Algiers.
Rais Kikwete pia alilaani tabia ya
makocha kufukuzwa baada ya timu
kufungwa. “Huku kwetu timu
ikifungwa, kocha anafukuzwa. Sasa
mnacheza na Algeria, ni timu bora
Afrika, timu ambayo ilifanya vizuri
zaidi ya zote kwenye Kombe la Dunia
mwaka jana,”alisema.
Aidha, Rais Kikwete amesistiza kocha
mzalendo Mkwasa, alipwe kama
ambavyo walikuwa wanalipwa
makocha wa kigeni. “Siyo kwa sababu
Mluguru tu wa Morogoro basi,
asilipwe vizuri,”alisema.
Toka bin zubeiry.



Chapisha Maoni