Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Mshambuliaji wa timu ya Simba, Hamisi Kiiza
ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa
mwezi Septemba.
Kwa kuibuka mchezaji bora, Kiiza atazawadiwa
sh. milioni moja kutoka kwa mdhamini wa Ligi
hiyo, kampuni ya Vodacom.
Kiiza ambaye ameisadia Simba kufanya vizuri
kwenye mwezi huo, ikiwemo kufunga mabao
matatu (hat trick) kwenye mechi dhidi ya Kagera
Sugar aliwashinda washambuliaji wa timu za
Stand United (Elias Maguli) na Yanga (Amisi
Tambwe).
Ndani ya mwezi Septemba ambapo zilichezwa
raundi tano, Kiiza amefunga jumla ya mabao
matano.
IMETOLEWA NA TFF

Hamis Kiiza (kulia) na Said Ndemla wa Simba,
wakishangilia bao la tatu aliloifungia timu yake,
wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom
dhidi Kagera Sugar, Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam leo. Simba imeshinda mabao 3-1,
yaliyofungwa na Kiiza.



Chapisha Maoni