Leo michuano ya klabu bingwa barani Ulaya
inaendelea kwa mechi kadhaa za makundi
kupigwa, mchezo ambao umeteka masikio na
macho ya wapenda soka wengi duniani ni ule
kati ya Arsenal dhidi ya Bayern Munich
utakaopigwa kwenye dimba la Emirates. Arsenal wanahitaji ushindi dhidi ya Bayern
Munich ili kujitengenezea mazingira ya kufuzu
hatua ya makundi kwenda hatua ya mtoano.
Wakati huo wanacheza na Bayern timu ambayo
imecheza michezo 12 kwenye mashindano yote
bila kupoteza hata mchezo mmoja. Mshambuliaji wa Bayern Robert Lewandowski
yuko kwenye ubora wa hali ya juu katika
kupachika mabao, lakini pia kwa upande wa
Arsenal wanajivunia Alexis Sanchez ambaye pia
yupo kwenye kiwango kiuri cha kutupia nyavuni. Arsenal inakutana na Bayern ikiwa imepoteza
michezo yake miwili ya UEFA Champions
League dhidi ya Dinamo Zagreb na Olympiacos.
Timu hizo zimekutana mara mbili mfululizo
kwenye hatua ya 16 bora misimu ya 2012-13
and 2013-14 na mara zote Arsenal imekua
ikiondolewa kwenye mashindano hayo. Hizi hapa ni rekodi za Arsenal na Bayern
Munich kwenye baadhi ya michezo ambayo
wameshakutana.
Asante kwa kutembelea Hope FM Iringa, Asante kwaku-share habari hii, Kama una Maoni, Ushauri, Story ya ku-share na sisi na au Unahitaji msaada...!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni