Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Mechi za raundi ya 11 za
Ligi Kuu Bara zilizokuwa
zichezwe Novemba 7 na 8
mwaka huu sasa zitafanyika
Desemba 12 na 13 kupisha
maandalizi ya Taifa Stars
ya mechi za mchujo za Kombe
la Dunia.
Taifa Stars inatarajia kuingia kambini
mapema mwezi ujao kujiandaa na mechi
ya kwanza dhidi ya Algeria ambayo
itafanyika Novemba 14 mwaka huu
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Timu hizo zitarudiana nchini Algeria,
Novemba 17 mwaka huu.
Mechi hizo za Vodacom
zitakazochezwa Desemba 12
ni kati ya Mgambo Shooting
na Yanga (Tanga), Kagera
Sugar na Ndanda (Tabora),
Stand United na Mwadui
(Shinyanga), Mbeya City na
Mtibwa Sugar (Mbeya), Azam
na Simba (Dar es Salaam) na
Majimaji na Toto Africans
(Songea). Mechi za Desemba
13 ni kati ya JKT Ruvu na
Tanzania Prisons (Dar es
Salaam), na Coastal Union
na African Sports (Tanga).
Pia mechi tatu za raundi ya
sita ambazo hazikuchezwa
Oktoba 4 mwaka huu kupisha
mechi ya Taifa Stars na
Malawi sasa zitafanyika
Desemba 16 mwaka huu. Mechi
hizo ni kati ya Azam na
Mtibwa Sugar (Dar es
Salaam), na African Sports
na Yanga (Tanga), mchezo
kati ya Ndanda na Simba
(Mtwara utapangiwa tarehe
ya kuchezwa.



Chapisha Maoni