Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Kocha Mkuu wa timu ya Taifa
‘Taifa Stars’, Charles
Boniface Mkwasa ametangaza
kikosi cha timu ya taifa
kilicho tayari kupambana na
Algeria.
Stars itaivaa Algeria katika mechi mbili
mfululizo kuwania kucheza Kombe la
Dunia 2018, ikianza kwa kupambana nayo
Novemba 17 jijini Dar es Salaam kabla ya
kurudiana Novemba 17, ugenini.
Akizungumza na waandishi wa
habari katika hoteli ya
Serena jijini Dar es
salaam, Mkwasa amesema
kikosi chake hicho kitaweka
kambi nchini Omani kwa
takribani siku 10 kujiandaa
na mchezo huo.
Kikosi kamili alichokitaja
Mkwasa kina wachezaji
wapya sita ambao Salim
Mbonde, Jonas Mkude, Salum
Abubakar, Malimi Busungu,
Ramadhani Kessy na Salum
Abubakary ‘Sure Boy’ na
kufanya idadi ya wachezaji
28.
Wachezaji aliowaita ni
Magolikipa ni Ally Mustafa
(Yanga), Aishi Manula
(Azam), Said Mohamed
(Mtibwa Sugar), walinzi wa
pembeni Kessy Ramadhani,
Mohamed Hussein (Simba),
Juma Abdul, Haji Mwinyi
(Yanga) na Shomari Kapombe
(Azam), Walinzi wa kati ni
Salim Mbonde (Mtibwa
Sugar), Hassan Isihaka
(Simba), Kelvin Yondani na
nahodha Nadir Haroub
(Yanga).
Viungo ni Salum Telela
(Yanga), Salum Abubakar,
Himid Mao, Mudathir Yahya,
Frank Domayo (Azam), Jonas
Mkude na Said Ndemla
(Simba), washambuliaji wa
pembeni Farid Musa (Aza



Chapisha Maoni