Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Klabu ya Liverpool inakaribia kumteua meneja
wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund
Jurgen Klopp.
Majogoo hao wa jiji la Liverpool wanatarajiwa
kukamilisha makubaliano yao siku ya Alhamisi na
Klopp raia wa Ujerumani kuchukua rasmi mikoba
ya Brendan Rodgers mwishoni mwa juma hili,
kwa mkataba wa miaka mitatu.
Rodgers alitimuliwa siku ya Jumapili kufuatia
suluhu ya 1-1 dhidi ya Everton katika mchezo wa
ligi kuu ya England.
Klopp ameomba kuambatana na wasaidizi wake
wawili wa zamani katika benchi la ufundi ambao
ni Zeljko Buvac na Peter Krawietz.
Buvac raia wa Bosnia mwenye miaka 54 na
mjerumani Krawietz mwenye miaka 43, walitoa
ushirikiano mzuri na kupata mafanikio makubwa
wakifanya kazi pamoja klabuni Borussia
Dortmund.



Chapisha Maoni