Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Mbwana Samatta
Jina kamili Mbwana Aly Samatta
tarehe ya kuzaliwa 7 Januari 1992 (umri 23)
mahali pa kuzaliwa Dar es Salaam, Tanzania

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania
anaecheza soka la kulipwa kwenye klabu ya TP
Mazembe ya nchini Congo DR amesema
hatoshangaa endapo mashabiki wa soka nchini
watawalaumu wachezaji wa Stars kwa
kushindwa kuifunga Malawi kwenye mchezo wa
leo.
Samata amesema Stars inabidi ishinde mchezo
wake wa leo dhidi ya Malawi kwasababu
viwango vya timu zote mbili vinalingana kwa
kiasi kikubwa. Licha ya kusema Stars ni lazima
ishinde mbele ya Malawi, lakini amesisitiza
kuwa inabidi ishinde kwa idadi kubwa ya magoli
huku yeye akikataa kuahidi chochote kwenye
mchezo huo.
“Siwezi kuahidi chochote kwasababu ahadi ni
deni na usipolitimiza ni dhambi, ila nadhani
kwamba tunaenda kupambana na siichukulii
Malawi kama Nigeria, nafikiri Malawi ni timu ya
kiwango chetu na nita-appreciate watanzania
kama watatulaumu kwanini hatujaifunga
Malawi”, amesema Samatta ambaye tayari
ameshafunga magoli sita baada ya kucheza
mechi nane kwenye ligi ya vilabu bingwa barani
Afrika.
“Lazima tuifunge Malawi hakuna matokeo
mengine ambayo tunayataka na ni lazima
tumfunge kwa idadi kubwa ya magoli, yani
lazima iwe hivyo”, amesisitiza Samatta ambaye
anatarajia kucheza fainali ya ligi ya mabingwa
Afrika siku chache zijazo akiwa na TP
Mazembe.

RECOD YA STARS MECHI 11 ZILIZOPITA.

: Swaziland 1-1 Tanzania
15: Tanzania 1-1 Malawi
: Tanzania 0-1 Swaziland
: Madagascar 2-0 Tanzania
esotho 1-0 Tanzania
Rwanda 2-0 Tanzania
: Misri 3-0 Tanzania
: Tanzania 0-3 Uganda
: Uganda 1-1 Tanzania
15: Tanzania 1-2 Libya
5, 2015: Tanzania 0-0 Nigeria



Chapisha Maoni