Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Rais wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Jamal
Malinzi ametuma salam za
pongezi kwa Alberto Simago
Junior wa Shirikisho la
Soka la Msumbiji (FMF) na
Sidiki Tombi wa Shirikisho
la Soka Cameroon (FECAFOOT)
kufuatia kuchaguliwa kuwa
marais wa mashiriksho hayo.
Katika salam zake kwenda
FMF na FECAFOOT, Malinzi
amesema kuchaguliwa kwao
kuogoza mashirikisho hayo
kumetokana na imani ya
wanafamilia wa mpira miguu.
Kwa niaba ya Kamati ya
Utendaji ya TFF na familia
ya mpira wa miguu nchini,
anawapa pongezi kwa
kucgahuliwa kwao.
TFF inaahidi kushirikiana
na uongozi mpya wa FMF na
FECFOOT katika maendeleo ya
mpira wa miguu Afrika na
Dunia kote.



Chapisha Maoni