Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Ligi Daraja la Kwanza
nchini (StarTimes First
League) inaendelea wikiendi
hii kwa makundi yote matatu
kucheza, michezo 11
itachezwa mwishoni mwa wiki
siku za Jumamosi na Jumapili
katika viwanja mbalimbali
nchini.
Jumamosi Kundi A, Ashanti
United watakua wenyeji wa
Mji Mkuu (CDA) katika
uwanja wa Karume jijini Dar
es salaam, KMC
watawakaribisha Polisi
Dodoma katika uwanja wa
Mabatini – Mlandizi.
Kundi B, Lipuli FC
watawakaribisha Polisi
Morogoro katika uwanja wa
Wambi mkoani Iringa,
Kimondo FC watakuwa wenyeji
wa JKT Mlale kwenye uwanja
wa CCM Vwava – Mbozi, huku
Burkinafaso ya Morogoro
ikiwakaribisha Njombe Mji
katika uwanja wa Jamhuri.
Kundi C, JKT Kanembwa
watakuwa wenyeji wa Panone
FC katika uwanja wa Jamhuri
mjini Dodoma, JKT Oljoro
watawakaribisha Polisi Moro
uwanja wa Sheikh Amri Abeid
jijini Arusha, Geita Gold
watacheza na Rhino Rangers
uwanja wa Nyankumbu mkoani
Geita na Polisi Tabora
watawakaribsiha Mbao FC
mjini Tabora uwanja wa Ali
Hassa Mwinyi.
Ligi hiyo itaendelea siku
ya Jumapili kwa michezo
miwili ya Kundi A, Friends
Rangers watacheza dhidi ya
African Lyon uwanja wa
Karume jijini Dar es
salaam, na Polisi Dar
watakua wenyeji wa Kiluvya
FC katika uwanja wa
Mabatini Mlandizi.



Chapisha Maoni