Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City
Sergio Aguero anatarajiwa kukaa nje kwa mwezi
mmoja baada ya kupata jeraha nyuma ya goti
lake wakati alipokuwa akiichezea Argentina.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27,ambaye
alifunga mabao matano pekee katika ushindi wa
klabu ya City dhidi ya Newcastle wikiendi iliopita
,alicheza kwa dakika 22 pekee wakati timu
Argentina iliposhindwa na Ecuador.
''Nadhani nitakuwa nje kwa kipindi cha mwezi
mmoja'' ,Aguero aliiambia TYC Sport katika mji
mkuu wa Bueno Aires.
Matatizo ya City vilevile yaliongezeka baada ya
David Silva kutoka katika mechi ya ushindi wa
4-0 dhidi ya Luxembourg baada ya kuteguka
kifundo cha mguu.



Chapisha Maoni