Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Kikosi cha timu ya Taifa ya
Tanzania (Taifa Stars)
kinachodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro Premieum Lager
kimewasili salama katika
mji wa Blantyre nchini
Malawi jioni ya  tayari
kwa mchezo wa Jumapili.
Stars inayonolewa na makocha wazawa
Charles Boniface Mkwasa na Hemedi
Morocco iliondoka leo kwa usafiri wa
shirika la ndege la Fastjet na kuwasili jiji la
Lilongwe saa 4 asubuhi kabla ya kuanza
safari ya bus kuelekea Blantayre
iliyochukua takribani masaa 3.
Wachezaji wote wapo katika
hali nzuri kuelekea katika
mchezo wa marudiano dhidi
ya Malawi siku ya Jumapili
ambapo Stars itashuka
dimbani kusaka matokeo
mazuri yatakayoiwezesha
kufuzu kwa hatua ya pili,
katika mchezo wa awali
uliochezwa jijini Dar es
salaam, Stars iliibuka na
ushindi wa mabao 2- 0.
Stars inatarajiwa kufanya
mazoezi kesho jioni katika
uwanja wa Kamuzu Banda
uliopo Blantyre, uwanja
ambao utatumika kwa mchezo
wa siku ya Jumapili.
Kuelekea mchezo huo wa
marudiano, Kocha wa Stars
Charles Mwasa amesema
vijana wake wote wapo
katika hali nzuri kiafya,
kifikra na morali ni ya
hali ya juu kuelekea kwenye
mchezo huo.
Katika hatua nyingine mabus
mawili yenye washabiki wa
Stars Supporter yako njiani
kuelekea nchini Malawi kwa
ajili ya kuipa sapoti timu
ya Taifa (Taifa Stars)
katika mchezo huo wa
Jumapili.



Chapisha Maoni