Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


BECHI la ufundi la timu ya Maji Maji limejipanga kuinoa zaidi safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ili kujihakikishia uwingi wa mabao katika mechi zijazo.

Katika mechi 6 ambazo timu hiyo imecheza timu ya Maji Maji imeshinda mechi mbili,sare moja kisha imepoteza mechi tatu huku safu ya ushambuliaji ya timu  imepachika wavuni bao tatu pekee hali ambayo imeanza kutishia uwezekano wa timu ya maji maji kufanya vizuri kwa siku za usoni.

Meneja wa timu hiyo God Mvula amesema ili Maji Maji ifikie malengo yake lazima kila idara ifanye kazi kama walivyokubaliana.

"Kikubwa ni wachezaji  kujituma ili kufikia malengo yao na timu,pia sisi viongozi tumejipanga kutekeleza majukumu ya timu ipasavyo ili kumaliza katika nafasi za juu.

Timu ya Maji Maji ambayo imepanda ligi kuu msimu huu mara baada ya kusota misimu mitatu inaitaji kutumia nguvu na maarifa ili kurudisha makali yake ya miaka ya 1980.



Chapisha Maoni