Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Liverpool imemfukuza kazi Meneja wao Brendan Rodgers kuanzia Leo mara tu baada ya kutoka Sare 1-1 na Everton kwenye Dabi ya Merseyside ya Mahasimu hao wa Jiji la Liverpool.

Matokeo haya ya Leo yameiacha Liverpool ikiwa Nafasi ya 10 kwenye Ligi Kuu England ikiwa Pointi 6 nyuma ya Vinara wa Ligi Man City.

Uamuzi huu wa umethibitishwa na Klabu ya Liverpool ambayo imetoa tamko kuwa wameanza kusaka Meneja mpya lakini tetesi ni kuwa Carlo Ancelotti, Frank de Boer na Jurgen Klopp wamehusishwa na kazi hiyo.

Brendan Rodgers alihamia Liverpool Juni 2012 na kuifikisha Nafasi ya Pili kwenye Msimu wa 2013/14 ambao waliongoza Ligi hadi zimebaki Mechi 3 na kupitwa na Manchester City.

Uamuzi wa kumtimua Rodgers ulifikishwa kwa Meneja huyo na Mtendaji Mkuu wa Liverpool, Ian Ayre, mara tu baada ya Mechi yao ya Leo na Everton kufuatia amri ya Wamiliki wa Liverpool ambao ni Fenway Sports Group ambayo Mmiliki wake mkuu ni Mmarekani John W Henry.

Kwa ajili ya Msimu huu, Liverpool ilitumia takriban Pauni Milioni 80 kuwanunua Wachezaji ambao ni pamoja na Christian Benteke, Danny Ings, Roberto Firmino, Nathaniel Clyne na Joe Gomez lakini hadi sasa wameshinda Mechi 4 tu baada ya Mechi 11 za Mashindano yote ikiwemo ile ya kushinda kwa Mikwaju ya Penati dhidi ya Timu ya Daraja la chini, Ligi 2, Carlisle, kwenye Mechi ya



Chapisha Maoni