Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) leo
limeingia mkataba wa miaka mitatu wenye
thamani ya shilingi milioni mia nne hamsini
(450,000,000), na kituo cha luninga cha Star Tv
kurusha matangazo ya Ligi Daraja la Kwanza
nchini (FDL).
Akiongea na waandishi wa habari wakati wa
kusaini mkataba huo, Rais wa TFF Jamal Malinzi
aliishukuru kampuni ya Sahara Media Group kwa
kuamua kuwekeza katika mpira wa miguu nchini
kwa kuamua kuonyesha ligi daraja la kwanza.
Malinzi ameviomba vilabu vya FDL kutumia
udhamini huo kama chachu ya mafanikio na
kufanya vizuri katika ligi hiyo itakayotoa timu tatu
za kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (FDL) msimu
ujao.
Aidha Malinzi amewaomba wamiliki wa viwanja
vinavyotumika kwa michezo ya FDL kuviweka
katika hali nzuri ya matunzo ili mechi
zinazochezwa katika viwanja hivyo ziweze kuwa
nzuri kiufundi na muonekano wa kwenye Luninga.
Jumla ya udhamini wa Ligi Daraja la Kwanza kwa
sasa ni shilingi bilioni moja na milioni mia tatu
hamsini (1,350,000,000) ikiwa ni udhamini wa
milioni mia tisa (900,000,000) kutoka StarTimes
mdhamini mkuu wa FDL na milioni mia nne
hamsini (450,000,000) kutoka StarTv.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Sahara Media
Group, Samwel Nyala ameishukuru TFF kwa
kuwapa nafasi hiyo ya haki za matangazo
kampuni yake kwa michezo ya Ligi Daraja la
kwanza nchini (FDL).
Katika kuhakikisha michezo hiyo inaonekana kwa
wingi zaidi, Nyala alisema watafungua mkondo
(Channel) ya Star Sports Plus itakayokua
itakayokuwa inaonyesha michezo tu ikiwemo ligi
daraja la kwanza (FDL).
Akiongea kwa niaba ya vilabu ya ligi daraja la
kwnza nchini (FDL), Asha Kigundula - Afisa habari
wa klabu ya Friends Rangers ya jijini Dar es
salaam, ameishukuru TFF kwa kuweza kuwapatia
udhamini kwenye ligi, jambo ambalo
litawapelekea kujiandaa na kufanya vizuri katika
ligi msimu huu.
IMETOLEWA NA TFF



Chapisha Maoni