Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Yale yake unaweza kusema hivyo
baada ya mchezaji wa timu ya taifa
ya mchezo wa raga ya Afrika Kusini
kumng’ata mwenzake.
Kupitia picha iliyopigwa na Kevin
Quigley, inaonyesha mchezaji wa
Afrika Kusini ‘Springboks’, Frans
Malherbe akididimiza meno yake
kwneye bega la Matt Trouville wa
timu ya taifa ya Marekani wakati
wakiwania mpira.
Usisahau, siku chache zilizopita
kumekuwa na gumzo la beki wa
Mbeya City, Juma Nyosso
kumtomasa makalio nahodha wa
Azam FC, John Bocco. Tayari
Nyosso amekumbana na adhabu ya
kufungiwa miaka miwili na faini ya
Sh milioni 2.
Hata hivyo, kitu kizuri zaidi, Trouville
ambaye aling’atwa amewaeleza
waamuzi kwamba hakumbuki
kuhusiana na tukio hilo kwa kuwa
alikuwa amevaa kifaa maalum cha
kulinda mabega ambacho huvaliwa
an wachezaji wa mchezo huo.
Bado haijajulikana kama Malherbe
atakumbana na adhabu, au suala la
muhusika yaani aliyeumwa kusema
hakumbuki, linaweza kumuokoa.

Source saleh jembe



Chapisha Maoni