Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Mamlaka za uendeshaji Kesi huko Spain
zimeamua kumfutia Mashitaka Lionel Messi ya
ukwepaji Kodi.
Mamlaka hizo zimetoa uamuzi huo baada ya
kuafiki hoja kwamba wakati makosa hayo
yakitendeka Messi alikuwa na umri mdogo kiasi
cha kutojua nini kinaendelea.
Hata hivyo Kesi hiyo itaendelea kwa Baba yake
Messi aitwae Jorge Messi.
Messi, ambae ni Mchezaji wa Barcelona,
alishtakiwa yeye pamoja na Baba yake kwa
ukwepaji Kodi kati ya 2007 na 2009 unaokadiriwa
kufikia Euro Milioni 4.1.
Ukwepaji huo wa Kodi ni ule wa kuuza Haki za
Matangazo ya Staa huyo nje ya Spain na hivyo
kuikosesha Nchi hiyo mapato.
Licha ya kumfutia Mashitaka Messi, Waendesha
Mashitaka wa Kesi hiyo wamesema Messi
huenda akaitwa Mahakamani kutoa ushahidi dhidi
ya Baba yake ambae ndie Wakala wake tangu
aanze Soka.
Ikiwa atapatikana na hatia, Jorge Messi anaweza
kufungwa Miezi 18 au kupigwa Faini Euro Milioni
2 au vyote kwa pamoja.
Hata hivyo, mara baada ya tuhuma hizi kuibuka
Messi na Baba yake walilipa Kodi yote
waliyokuwa wakidaiwa pamoja na malimbikizo ya
Riba yake.



Chapisha Maoni